Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda

Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda
kiungo : Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda

soma pia


Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda

Na Mwandishi Wetu, Dar
BENKI ya Azania imeahidi kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Tano katika kuhakikisha uchumi wa viwanda unafanikiwa kwa kuwezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa kutimiza malengo yao katika .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azania Bank, Charles Itembe alisema benki yao imeendelea kutengeneza faida kutokana na kujihusisha kwa kiasi kikubwa kutimiza matakwa ya wateja wao.

“Tunatambua umuhimu wa malighafi katika uchumi wa viwanda, ndiyo mana tuna utaratibu maalumu wa mikopo kwa ajili ya wakulima kwa sababu bidhaa zinahitaji malighafi ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na wakulima,” alisema Itembe.

Amesema  katika ripoti yabenki hiyo ya mwaka 2017 wamepata matokeo mazuri ingawa baadhi ya benki zilipata misukosuko katika uwekezaji.  Pia amebainisha wamepata faida ya Sh bilioni 1.8 kinyume na hasara waliyoipata mwaka mmoja uliopita.

Katika kuonyesha benki hiyo ipo kwa ajili ya kuinua wajasiriamali Itembe amesema mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kiasi kikubwa ndio wanaoiendesha kwa kuwa na uwekezaji wa zaidi ya asilimia 90 hali inayoonyesha inamilikiwa na wananchi.

“Kuna ongezeko la mapato halisi ya faida ya Sh milioni 25,056 kwa mwaka 2017 kutoka ongezeko la faida la Sh milioni 22,100 iliyorikodiwa kwa mwaka 2016. Amana zimeongezeka kwa asilimia 14.8 kutoka Sh bilioni 236,380 zilizoainishwa Disemba 2016 hadi Sh bilioni 271.3 Disemba 2017,” alisema Bw. Itembe.

Aliweka wazi kuwa mafanikio hayo katika biashara yametokana na kuwa karibu na wateja wao lakini pia mipango na mikakati waliyojiwekea katika uendeshaji shughuli za kibenki ikiwemo kuhakikisha benki hiyo inakuwa kituo kinachotoa huduma zote za kifedha.

“Hii ni benki inayomilikiwa kwa zaidi ya asilimi 90 na mifuko ya hifdhi ya jamii maana yake inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na wananchi ambao wanatoa michango katika benki hizo.  Katika kudhihirisha hilo mifuko hii imetoa  ongezeko la uwekezaji wa asilimia 91.1 kwa kiasicha Sh bilioni 57,881 December, 2017; kutoka Sh bilioni 30,058 Disemba mwaka 2016,” alisema Bw. Itembe.

Akitoa historia fupi ya benki hiyo, Bwana Itembe aliema: “Azania Bank ilianzishwa mwaka 1995 wakati Tanzania ilipoamua kwa na mfumo huria wa benki, ikiwa na wawekezaji 47  ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii ambayo hadi sasa inamiliki asilimia 98 ya hisa zote ikiongozwa na NSSF inayomiliki asilimia 35.8, Benki ya Maendeleo ya Afrika Mashariki (EADB)  asilimia 1.5 na wawekezaji  wengine asilimia 0.93.”

Ofisa Mtendaji Mkuu huyo wa Azania Bank amesisitiza kuwa ikiwa mtu ataweka fedha zake katika benkihiyo atakuwa amegeneza afya ya mafao yake ya baadaye kwa sababu mifuko ya jamii ina hisa nyingi na kuweka wazi kuwa wanataka kuwa kitovu cha huduma za fedha nchini.

Sekta ya fedha nchini imekumbwa na changamoto ya kuwa na mitaji midogo na kutengeneza hasara kutokana na masuala mbalimbali yatokanayo na mazingira ya biashara, lakini benki ya Azania imedhamiria kujikita katika kusaidia wananchi ambapo inadai ndio wanaoiendesha kupitia mifuko ya jamii.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azania Bank, Charles Itembe akizungumza na waandishi wa habari kuhusu benki yao ilivyoendelea kutengeneza faida kutokana na kujikita zaidi kwenye sekta ya viwanda kwa kuwezesha wajasiriamali wadogo na wakubwa kutimiza malengo.


Hivyo makala Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda

yaani makala yote Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/benki-ya-azania-yaahidi-kusaidia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Benki ya Azania yaahidi kusaidia kutimia uchumi wa viwanda"

Post a Comment