title : ADC AMA "MPAMBE" WA RAIS NI NANI?
kiungo : ADC AMA "MPAMBE" WA RAIS NI NANI?
ADC AMA "MPAMBE" WA RAIS NI NANI?
Kufuatia kupandishwa cheo kwa aliyekuwa Msaidizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania (JWTZ) Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Kanali M.N Mkeremy kuwa Brigedia Jenerali na nafasi yake kuchukuliwa na Kanali B.M Mlunga aliyepandishwa kutoka Luteni Kanali kuwa Kanali hapo jana, Uwanja wa Diplomasia tumeona turejee maelezo yetu juu ya maana ya ADC ili jamii ipate kunufaika.
TUELIMIKE
Kwa kawaida kila tumuonapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli nyuma yake huwa amesimama Afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Uwanja wa Diplomasia tumekuwa tukiulizwa maswali sana juu ya mtaalamu huyo wa Jeshi lakini tumekuwa tukisita kwa kuhofia kuingilia majukumu ya watu.
Tulipoona maswali yanazidi ilibidi tuwasiliane na wahusika ili tuweze kufahamu kama tukitoa elimu juu ya hili tutakuwa tumechupa mipaka ama la. Leo Uwanja wa Diplomasia tunakuletea maelezo kidogo juu ya afisa huyu wa jeshi (JWTZ).
AFISA HUYU KIITIFAKI ANAITWAJE?
Afisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ambaye huwa amesimama nyuma ya Rais akiwa na suti ya kijeshi ama kombati kiitifaki hutambulika kama ADC.
ADC ama A de C ni cheo cha heshima ambacho hutunukiwa Msaidizi Mkuu wa kiongozi wa Juu wa Nchi kama Rais, Mfalme ama Malkia. Kirefu cha ADC ni Aide de Camp neno ambalo kwa Kiswahili hujulikana kama Msaidizi (wa Kambi). Neno hili limetoka katika mazingira ya kijeshi kwa kuwa nchi karibu zote duniani zimetokana na vita.
ADC wa Rais huweza kuwa afisa wa ngazi ya juu kuanzia cheo cha Meja, Luteni Kanali au Kanali kulingana na hadhi ya nchi kimataifa na anapofika cheo cha Brigedia Jenerali hupangiwa majukumu mengine.
Mara nyingi ADC wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huwa ni Afisa wa ngazi ya juu wa Jeshi mwenye cheo cha Kanali wakati kwa upande wa Tanzania Visiwani huwa ni Luteni Kanali. Hii ni kutokana na hadhi ya Tanzania kimataifa.
Si Rais tu pekee huwa na ADC bali Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama CDF ana ADC wake, Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP ana ADC wake na hata Mkuu wa Jeshi la Magereza CGP na Uhamiaji CGI huwa na maADC zao.
KAZI ZA ADC WA RAIS NI HIZI ZIFUATAZO:
ADC wa Rais ana kazi nyingi sana kutokana na kuwa kwake Msaidizi Mkuu wa Rais, kazi hizo ni kama zifuatavyo;
(1) Msaidizi Mkuu wa kazi za kila siku ofisi ya Rais.
(2) Huandaa kalenda, ratiba na safari za Rais.
(3) Huandaa masuala yote ya kiitifaki ya Rais.
(4) Hupokea wageni wa Rais.
(5) Hupokea zawadi mbalimbali kama ngao,mikuki n.k ambayo Rais hupewa kama zawadi akiwa ziarani.
(6) Humbebea Rais Begi/Mkoba wake sambamba na diary na peni.
(7) Huwaongoza na kuwaelekeza staff wengine.
(8) Hufanya kazi mbalimbali kwa mujibu wa muongozo dawati la ofisi ya Rais.
(9) Husimamia e-mails sambamba na kuandaa na kupitia mawasiliano yote ya kiofisi ya Rais.
(10) Husaidia kuandaa safari, kusalimia wageni, mabalozi na kusoma ramani.
Uwanja wa Diplomasia tumewaletea maelezo ya mambo ama shughuli za kila siku za ADC ambazo tunaamini zitakuwa zimefungua uelewa wenu wote mliouliza.
Karibuni tuendelee kuelimishana.
Abbas Mwalimu.
+255 719 258 484.
Uwanja wa Diplomasia (Facebook)
Hivyo makala ADC AMA "MPAMBE" WA RAIS NI NANI?
yaani makala yote ADC AMA "MPAMBE" WA RAIS NI NANI? Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ADC AMA "MPAMBE" WA RAIS NI NANI? mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/04/adc-ama-mpambe-wa-rais-ni-nani.html
0 Response to "ADC AMA "MPAMBE" WA RAIS NI NANI?"
Post a Comment