title : Zanzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA
kiungo : Zanzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA
Zanzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA umeteketeza kwa moto kilo 48 za Nyama kutoka Afrika Kusini ambazo ziliingizwa nchini kinyume na sheria.
Nyama hizo zilizokuwa mali ya Kampuni ya Qamar ya Vingunguti jijini Dar es Salaam zilikamatwa Uwanjwa wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza katika zoezi hilo Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa hatari zinazotokana na Chakula Aisha Suleiman amesema kilichosababisha kuteketezwa kwa nyama hizo ni katazo lililotolewa na ZFDA yenye majukumu ya kuhakikisha wananchi wanapata Chakula na Dawa zilizokuwa salama.
Amesema maamuzi ya katazo hilo yametokana na uwepo wa maradhi ya mripuko ya Listeria nchini Afrika Kusini hivyo Ofisi yao ikapiga marufuku uingizwaji wa Nyama, Maziwa na Samaki kutoka nchi hiyo.
Amesema katazo hilo si kwa Zanzibar pekee bali pia Tanzania bara na nchi nyingine kutokana na utaratibu wa biashara kimataifa.
Nyama kutoka Afrika ya kusini zilizoingizwa Zanzibar kinyume na sheria na Kampuni ya Qamar zikiwa zimewekwa katika Maboksi kabla ya kuteketezwa huko Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Mkuu wa Jiko la kuteketezea bidhaa mbovu Khamis wa Khamis Mkanga akiziingiza nyama katika jiko hilo kwa ajili ya kuteketezwa baada ya kuingizwa nchini kinyume na sheria kutoka Afria ya Kusini. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Nyama kutoka Afrika ya kusini zilizoingizwa Zanzibar kinyume na sheria na Kampuni ya Qamar zikiwa zimeingizwa katika Jiko tayari kwa kuteketezwa huko Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja. Picha na Abdallah Omar-Maelezo Zanzibar
Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa hatari zinazotokana na Chakula kutoka Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar (ZFDA), Aisha Suleiman akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya zoezi la kuteketeza nyama zilizoingizwa nchini kinyume na Sheria na Kampuni ya Qamar ya Jijini Dar es Salaam kutoka Afrika ya Kusini.
Mkaguzi wa bidhaa za Chakula hususan Nyama, Daktari Othman Juma Othman akielezea ugonjwa wa Listeria na madhara yake mara baada ya zoezi la kuteketeza nyama kufanyika.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Zanzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA
yaani makala yote Zanzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Zanzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/zanzibar-yeteketeza-nyama-kutoka-afrika.html
0 Response to "Zanzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA"
Post a Comment