MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI

MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI
kiungo : MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI

soma pia


MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI


WANANCHI wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga wametakiwa kufanya subira wakati mgogoro wao wa fidia na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji madini ya Henan Afro Asian Engineering ukitafutiwa ufumbuzi.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ametoa wito huo Machi 12, 2018 kwenye mkutano na wananchi hao uliofanyikia kwenye Kitongoji cha Mahiga na kuhudhuriwa na watendaji mbalimbali wa Serikali.

Mkutano huo unafuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alilolitoa Machi 11, 2018 kwenye mkutano na wananchi wa Kahama ambapo alielezwa na Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum kuwa wananchi wa Mahiga wana mgogoro wa muda mrefu na mwekezaji hususan kuhusiana na suala la ulipaji fidia ili kupisha mradi.

Kufuatia maelezo hayo ya Mbunge, Rais Dkt. Magufuli alimuagiza Naibu Waziri Biteko kuhakikisha anafika kwenye eneo hilo ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi. 

Rais Magufuli alisisitiza kuwa ni wakati sasa Watanzania waanze kunufaika na rasilimali zao ikiwemo madini. "Tunataka madini yawanufaishe Watanzania," alisema Rais Magufuli.

Alisema wawekezaji wakifika nchini ni lazima wahakikishe Watanzania wananufaika kwa namna mbalimbali ikiwemo ajira, kodi na tozo.

"Jukumu langu nimeamua kusimamia suala hili; Nawahakikishia Serikali iko imara kwa ajili ya kuwatetea wanyonge," alisema Rais Dkt. Magufuli.
 Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akizungumza na wananchi wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo Wilayani Shinyanga (hawapo pichani) kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
 Wananchi wa Kijiji cha Mwakitolyo, Wilayani Shinyanga wakimsikiliza Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (hayupo pichani) akizungumza kuhusu mgogoro wao na Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.
 Mbunge wa Jimbo la Solwa, Ahmed Salum akizungumza na wananchi wake wa Kitongoji cha Mahiga, Kijiji cha Mwakitolyo, Tarafa ya Nindo Wilayani Shinyanga kuhusiana na mgogoro wao na mwekezaji ambaye ni Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Henan Afro Asian Engineering.


Hivyo makala MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI

yaani makala yote MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mgogoro-mwakitolyo-kupatiwa-ufumbui.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MGOGORO MWAKITOLYO KUPATIWA UFUMBUI"

Post a Comment