WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO

WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO
kiungo : WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO

soma pia


WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO

Na Hamza Temba, Dodoma

Wizara ya Maliasili na Utalii imeendesha warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


Akifungua warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini hapa jana, Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mradi huo unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na nchi ya Uswizi kupitia shirika la kiuchumi la State Secretariat for Economic Affairs-SECO.


Alisema mradi huo pia unalenga kuongeza ununuzi wa mazao na bidhaa za mbogamboga na matunda zinazozalishwa Tanzania, kuongeza  ajira kwa Watanzania waliojifunza vema masuala ya utalii, na kuongeza nafasi ya kujadili dhana ya Utalii Wenye Manufaa kwa jamii.


"Mradi huu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Umoja wa Mataifa zinazohusika na eneo la  Maendeleo ya Biashara (UN Trade Cluster Organizations) - UNIDO, UNCTAD, ITC na ILO, taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, na sekta binafsi" alisema Dk. Kigwangalla.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.


 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wiazara hiyo, Degracious Mdamu muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja  iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Ernest Mwamaja ambaye aliwasilisha mada katika warsha hiyo.

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.



Hivyo makala WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO

yaani makala yote WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wizara-ya-maliasili-yazijengea-uelewa_25.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WIZARA YA MALIASILI YAZIJENGEA UELEWA KAMATI MBILI ZA BUNGE KUHUSU MRADI WA SECO"

Post a Comment