title : WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI
kiungo : WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI
WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI
Na John Nditi, Morogoro
WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imesema ili kuleta ufanisi mkubwa katika usimamizi wa miradi ya maji safi na salama vijijini, ipo haja ya kuwa na chombo cha kusimamia huduma za maji vijijini utakaosimamiwa na wizara kwa lengo la kuleta uwajibikaji wa karibu kwa watumishi wanaosimamia sekta ya maji nchini.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Jumaa Aweso alisema hayo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali kikiwemo cha Dumila juu katika Kata ya Dumila, wilaya ya Kilosa, mkoani Morogoro.
Kabla ya kuzungumza na wananchi alipata fursa ya kukagua ujenzi wa mradi wa maji Dumila ambao ulianza kujengwa tangu Januari 24, 2014 na kukamilishwa Desemba 15, 2017 kwa gharama ya Sh milioni 800.5.
Naibu Waziri huyo alifanya ziara ya wiki moja mkoani Morogoro iliyomfikisha katika halmashauri za wilaya sita kati ya tisa ambazo ni Malinyi, Ulanga, Kilombero, Mvomero, Manispaa ya Morogoro na Kilosa .
Alisema kuwa, miradi mingi ya maji safi na salama inayotekelezwa vijijini imekosa usimamizi wa karibu, ufanisi na mingi imejengwa chini ya viwango na baadhi katika maeneo ambayo vyanzo vyake vya maji si vya kuaminika.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuwapelekea mafundi wa ujenzi kwa ajili ya ukamilishaji wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 katika mji wa Malinyi, ( kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda akichanganya saruji na mchanga kwa ajili ya ujenzi huo.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akisadia kuchanganya mchanga na saruji kwa ajili ya ukamilishaji wa hatua za mwisho ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 mjini Malinyi na ( kushoto kwake ) ni Mbunge wa Jimbo la Malinyi, Mkoani Morogoro, Dk Haji Mponda , na ( wa kwanza kushoto) ni Mkuu wa wilaya hiyo Majura Kasika.
Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaji , Jumaa Aweso, akimsiliza Mzee Said Mazinge wa Kata ya Kibati, wilaya ya Mvomero , mkoa wa Morogoro kuhusu changamoto za upatikanaji wa maji safi na salama alipofanya ziara wilayani Mvomero. .
Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso akiwahutubia wakazi wa mji wa Mlimba , wilaya ya Kilombero juu ya azma ya serikali ya awamu ya tano ya namna ya kutatua changamoto za ukosefu wa maji maeneo ya vijijini na mijini.
Naibu waziri wa Maji na Umwagiliaj, Jumaa Aweso akipambu maji katika moja ya kisima kirefu mara baada ya kukizundia katika kijiji cha Chikuti, wilaya ya Ulanga kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa kijiji hicho .
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI
yaani makala yote WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wizara-kuangalia-njia-sahihi-ya.html
0 Response to "WIZARA KUANGALIA NJIA SAHIHI YA UBORESHAJI UTOAJI HUDUMA ZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI"
Post a Comment