anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA

anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA
kiungo : anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA

soma pia


anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA





Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar 14.03.2018
Wakala wa Chakula na Dawa Zanzibar ZFDA umeteketeza kwa moto kilo 48 za Nyama kutoka Afrika Kusini ambazo ziliingizwa nchini kinyume na sheria.
Nyama hizo zilizokuwa mali ya Kampuni ya Qamar ya Vingunguti jijini Dar es Salaam zilikamatwa Uwanjwa wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume mwishoni mwa wiki iliyopita.
Akizungumza katika zoezi hilo Mkuu wa kitengo cha Uchambuzi wa hatari zinazotokana na Chakula Aisha Suleiman amesema kilichosababisha kuteketezwa kwa nyama hizo ni katazo lililotolewa na ZFDA yenye majukumu ya kuhakikisha wananchi wanapata Chakula na Dawa zilizokuwa salama.
Amesema maamuzi ya katazo hilo yametokana na uwepo wa maradhi ya mripuko ya Listeria nchini Afrika Kusini hivyo Ofisi yao ikapiga marufuku uingizwaji wa Nyama, Maziwa na Samaki kutoka nchi hiyo.
Amesema katazo hilo si kwa Zanzibar pekee bali pia Tanzania bara na nchi nyingine kutokana na utaratibu wa biashara kimataifa.
“Hili katazo siyo sisi tu ni utaratibu wa Kimataifa kwamba kutokana na Maradhi ya Listeria bidhaa za Nyama, Samaki, Maziwa ni marufuku kuingizwa nchini sasa hii Kampuni ya Qamar LTD ya Dar es Salaam wao waliamua kuingiza nyama hizo kwa hiyo tumezikamata na kuziangamaza.” Alisema Aisha.
Hivyo kwa lengo la kulinda wananchi wasipate matatizo wameamua kuitekekeza Nyama hiyo huko maeneo ya Kivunge Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Ametoa wito kwa Wafanyabiashara kufuata taratibu zilizowekwa kisheria na kufuatilia taarifa zinazotolewa na Wakala wa Chakula na Dawa ili kuhakikisha wanaingiza bidhaa salama kwa afya ya Wananchi wa Zanzibar.
Aidha amewaomba kufuatilia vyema taarifa za utandawazi ili kujua kinachoendelea Duniani.
Akielezea hatua zilizochukuliwa kwa Kampuni hiyo iliyoingiza nyama hizo amesema Kampuni imelazimishwa kulipia ngamarama zote za uteketezaji wa nyama hiyo na asilimia tano ya uingizaji wa bidhaa hiyo.
Kwa upande wake Mkaguzi wa bidhaa za Chakula hususan Nyama Daktari Othman Juma Othman akielezea ugonjwa wa Listeria amesema ugonjwa wa maambukizi unaosababishwa zaidi na Vimelea vya Bakteria ambapo hupatikana kwa kula vyakula vilivyoshambuliwa na Bakeria hao.
Ugonjwa huo wa mripuko huwaathiri zaidi Watoto na watu wazima ambao afya na kinga za mwili zimetetereka.
Aidha Mama wajawazito ni miongoni mwa waathika wakubwa wa ugonjwa huo na kuwasababishia kuharibu mimba zao pale ambapo utaingia nchini.
Nchini Afrika kusini Ungonjwa wa Listeria uligundulika rasmi mwezi November mwaka jana ambapo tayari umesababisha vifo vya zaidi ya watu 180.
Hivi karibuni Wakala wa Chkula na Dawa Zanzibar ZFDA ulikabidhiwa rasmi Cheti cha mfumo wa uhakikiki ubora wa huduma cha kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015 ikiwa ni kielelezo cha taasisi hiyo kusimamia misingi imara ya kuhakiki ubira wa huduma katika kiwango cha kimataifa.
Imetolewa na Maelezo


Hivyo makala anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA

yaani makala yote anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/anzibar-yeteketeza-nyama-kutoka-afrika.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "anzibar yeteketeza Nyama kutoka Afrika Kusini kuepuka Maradhi ya LISTERIA"

Post a Comment