title : WAZIRI WA MAJI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI, MAZINGIRA
kiungo : WAZIRI WA MAJI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI, MAZINGIRA
WAZIRI WA MAJI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI, MAZINGIRA
Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ni muhimu kuwekwa mikakati ya kukabiliana na uharibifu unaoendelea katika vyanzo mbalimbali vya maji na misitu nchini.
Mhandisi Kamwele amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani na kwa Tanzania lengo lake ni kuangalia uwezekano wa kuwapatia maji safi na salama kwa watanzania wote.
Aidha ameeleza mkakati wa kuvuna maji ya mvua ili kupata maji shuleni kupitia matanki na visima vya kujenga ambapo anaamini itasaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa maji shuleni.
Pia ameeleza mafanikio katika suala la maji na majengo katika shule za Kirumba na Isenyi jijini Mwanza pia katika ujenzi wa vyoo na vyumba kwa wanafunzi wa kike.
Ameshukuru Benki ya dunia, Serikali ya Korea na Mpango wa maendeleo Ufaransa kwa ushirikiano wao katika suala la maji na utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ni lazima.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wadau wa maji uliandaliwa na benki ya Dunia nchini uliokwenda kwa jina la 'TANZANIA WASH POVERTY DIAGNOSTIC' uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Malawi na Burundi, Bella Bird akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji kufungua mkutano huo muhimu kwa ajili ya maji Tanzania.
Mwasilishaji wa mada juu ya kupinga umaskini na uhaba wa maji Mchumi wa Benki ya Dunia, George Joseph akizungumza na wadau wa maji waliofika katika mkutano huo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini(TUDARCO), Prof. Uswege Minga akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa utunzaji wa maji na na mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAZIRI WA MAJI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI, MAZINGIRA
yaani makala yote WAZIRI WA MAJI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI, MAZINGIRA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI WA MAJI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI, MAZINGIRA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/waziri-wa-maji-azungumzia-umuhimu-wa.html
0 Response to "WAZIRI WA MAJI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI, MAZINGIRA"
Post a Comment