title : WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI WAFANYIWE UTAFITI WA KINA
kiungo : WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI WAFANYIWE UTAFITI WA KINA
WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI WAFANYIWE UTAFITI WA KINA
Wakati umefika wa kufanywa utafiti wa kina kujua mazingira halisi ya Watu wenye mahitaji Maalum Nchini ili kupata mwanga wa uhakika wa kuelewa pamoja na kuyatafutia ufumbuzi wa kudumu mahitaji wanayopaswa kupatikana kwa kundi hilo katika Jamii.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mheshimiwa Omar Seif Abeid alieleza hayo wakati akitoa Taarifa kwenye Kikao cha Majumuisho ya Ziara ya kamati hiyo hapo katika Ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar.
Mh. Omar alisema ushirikishwaji wa Watu wenye Mahitahi maalum yaani Walemavu bado ni mdogo hasa katika maeneo ya Vijiji jambo ambalo husababishwa kukumbwa na changamoto nyingi likiwemo wimbi la udhalilishwaji wa Kijinsia ambalo kwa sasa limeshika kasi na kuendelea kuwaathiri kiakili.
Alisema ipo haja kwa Taasisi za Umma kuendelea kuwatumia Masheha pamoja na Makundi ya Kioraia katika maeneo husika kuliona tatizo hili na kutafuta mbinu ya pamoja na kulitatua.
Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar chini ya Mwenyekjiti wake waliokaa kati kati Kulia Mheshimiwa Omar Seif Abeid wakiwa katika Kikao cha majumuisho ya ziara yao ndani ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kilichofanyika Vuga Mjini Zanzibar.
Baadhi ya watendaji Wakuu na Maafisa wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar walioshiriki katika Kikao hicho cha Majumuisho ya Kamati hiyo.
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kusimamia Ofisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakiwa katika Kikao hicho cha Majumuisho ya ziara yao ndani ya Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziba. Picha na – OMPR – ZNZ.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI WAFANYIWE UTAFITI WA KINA
yaani makala yote WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI WAFANYIWE UTAFITI WA KINA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI WAFANYIWE UTAFITI WA KINA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/watu-wenye-mahitaji-maalum-nchini.html



0 Response to "WATU WENYE MAHITAJI MAALUM NCHINI WAFANYIWE UTAFITI WA KINA"
Post a Comment