WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI

WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI
kiungo : WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI

soma pia


WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
WATETEZI wa Rasilimali wasio na Mipaka-WARAMI wameupinga waraka wa Ujumbe wa pasaka kutoka kwa baraza la maaskofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) uliotolewa jana, kwa madai kuwa ulikuwa wa kisiasa wenye lengo la kukososa utendaji wa serikali na kuleta hofu kwa jamii.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Da res Salaam, Mkurugenzi wa Utafiti WARAMI, Philipo Mwakibinga amedai kuwa maskofu kama viongozi wa dini wanatakiwa kujikita katika masuala yanayohusu dini na si siasa.

“WARAMI tunaamini kwamba wajibu wetu ni kuhakikisha jamii inapata haki pasipo upendeleo wowote, kufuatia hili tumeona si sahihi kukaa kimya, tukaona tupaze sauti kuona tunaijenga jamii kulingana na tofauti zao. Kwenye nafsi zao wanavyo vyama vyao mbali na uongozi wa kidini. Hisia za kivyama zisilete mtafaruku kwenye Imani. Wajitafakari kuchagua aina ya maneno wanayotoa kwa jamii ili kulinda na kukuza amani,” amesema na kuongeza.

“Tunashangaa kwa nini waraka huu wa salamu za pasaka haukujikita katika kuwasisitiza waumini wake kujikita katika kuabudu, kumnyenyekea Mungu, kusoma biblia na maandiko mengine ya dini na badala yake wanajikita katika maoni yanayong’ata na kupuliza.”

Mwakibinga amedai kuwa, Miongoni mwa masuala yaliyoandikwa katika waraka huo ni malalamiko kuhusu mchakato wa katiba mpya na uhuru wa kutoa maoni, ambao ulikwamishwa na wansiasa wa upinzani waliosusia kushiriki mchakato huo.  

“Maaskofu wamezungumzia kuhusu utekwaji na mauaji ikiwemo utiaji wa hofu lakini hawajajikita kuelezea kwa kina kisa hasa ni kipi. Sisi tunafahamu kuwa wapo walioathirika moja kwa moja na matukio ya kutekwa na kuteswa kwa baadhi ya vijana ambayo yalipaswa kukemewa tangu siku ya kwanza ya kutokea kwake na si kuyasubiri mpaka leo,” amesema.
 Mkurugenzi wa Utafiti   wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini.
Mkurugenzi wa Utafiti   wa Tasisi ya Watetezi wa Rasilimali wasio na Mipaka (WARAMI), Philipo Mwakibinga akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya kukosoa tamko lililotolewa na Maaskofu wa KKKT nchini katika ukumbi wa Traventine Magomeni.


Hivyo makala WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI

yaani makala yote WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/warami-wapingana-na-waraka-wa-maaskofu.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WARAMI WAPINGANA NA WARAKA WA MAASKOFU WA KKKT NCHINI"

Post a Comment