title : WAKURUGENZI WATANO TPDC WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA
kiungo : WAKURUGENZI WATANO TPDC WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA
WAKURUGENZI WATANO TPDC WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii
WAKURUGENZI watano wa Shirika la Maendeleo ya Petrol (TPDC), akiwemo, Mkurugenzi Mtendaji James Mataragio na wenzake wanne, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka ya zaidi ya Sh. bilioni 7.
Mbali na Mataragio, washtakiwa wengine ni, Mkurugenzi wa fedha, George Seni, Welington Hudson, Mkurugenzi wa mkondo wa juu, Kelvin Komba, na mkurugenzi wa manunuzi na Ugavi Edwin Riwa.
Akisoma hati ya mashtaka wakili wa Serikali kutoka Takukuru,leo mahakaman Emmanuel Jacob amedai, kati ya April 8/ 2015 na June 3 mwaka 2016 washtakiwa hao wakiwa watumishi wa umma na waajiriwa wa Shirika la Maendeleo la Petrol (TPDC), katika nafasi zao hizo za kazi walitenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.
Mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri imedaiwa, washtakiwa wakati wakitimiza majukumu yao ya kazi kwa makusudi walitumia madaraka yao vibaya kwa kubadirisha na kupitisha bajeti na mpango mkakati wa mwaka wa manunuzi na ugavi wa bajeti ya mwaka 2014/15 na 2015/16 kwa kuingiza ununuzi wa wa kifaa cha utafiti kiitwacho, air borne gravity gradiometer survey ndani ya ziwa Tanganyika bila kupata idhini kutoka kwa bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo, kitendo ambacho ni kinyume cha kifungu cha 49(2) cha sheria ya manunuzi ya umma ya 2011 kwa lengo la kujipatia manufaa yasiyo halali ya USD 3, 238,986.50 ambazo ni sawa na zaidi ya sh. Bilioni 7.2 for bellGeospace.
Hata hivyo, washtakiwa wote wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya mahakama waliyopewa na Mahakama.Mahakama imewataka kuwa na wadhamini wawili watakai saini bondi ya bilioni moja kila mmoja huku washtakiwa wenyewe nao wakitakiwa kusaini bondi hiyo ya bilioni moja.
Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika. Kesi hiyo itatajwa tena Aprili 19, mwaka huu.
Hivyo makala WAKURUGENZI WATANO TPDC WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA
yaani makala yote WAKURUGENZI WATANO TPDC WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAKURUGENZI WATANO TPDC WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wakurugenzi-watano-tpdc-wafikishwa.html
0 Response to "WAKURUGENZI WATANO TPDC WAFIKISHWA KORTINI KWA TUHUMA ZA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA"
Post a Comment