title : WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA
kiungo : WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA
WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA
Na Mwandishi Maalum
Jumla wa wagonjwa wa akili 55 waliokuwa wametenda makosa mbalimbali yakiwamo ya jinai wakiwa na ugonjwa wa akili, wameachiwa huru baada ya mahakama kutowatia hatiani.
Hayo yameelezwa leo mjini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi ( Mb) wakati alipokuwa akiwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara Katiba na Sheria na Taasisi zake kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria. Kamati hiyo ilikuwa nchini ya Uenyekiti wa Mhe. Najma Murtaza Gingo ( Mb). Waziri Kabudi ameieleza Kamati hiyo kwamba, kifungu cha 219 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai, Sura ya 20, kinampatia Waziri mwenye dhamana ya masuala ya sheria mamlaka ya kuwaachia huru wagonjwa wa akili waliotenda makosa mbalimbali ya jinai yakiwamo ya mauaji.
“ Kutokana na mamlaka hayo ya kisheria, katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, nilisaini hati ya kuachiliwa huru wagonjwa 55 wa akili waliotenda makosa mbalimbali ya jinai wakiwa na ugonjwa wa akili na hivyo mahakama kutowatia hatiani” akabainisha Waziri Kabudi.
Na kuongeza kwamba, kwa muda mrefu wagonjwa hao walikuwa wakihifadhiwa kwenye Taasisi ya Isanga kusubiri amri ya Waziri. "Na kutokana na hali ya afya zao za akili kuimarika, niliamua waachiliwe huru, ili waungane na familia zao na kuendelea na matibabu wakiwa nje ya taasisi hiyo”.
Pamoja na kuelezea kuachiwa huru kwa wagonjwa wa akili, Waziri Kabudi pia alianisha mafanikio mbalimbali yaliyotekelezwa na Wizara pamoja na Taasisi zake katika suala zima la utoaji na usimamiaji wa haki katika kipindi cha bajeti cha 2017/2018.Baadhi ya mafanikio hayo ni kwa Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika uendeshaji wa mashauri ya daawa ili pata ushindi katika mashauri 82 yaliyokuwa na thamani ya shilingi 1,064,581,955,743bn/-. Kwa mujibu wa Waziri wa Katiba na Sheria ushindi huo umewezesha pamoja na mambo mengine maamuzi ya serikali pamoja na sheria za nchi kutobadilishwa kwa msingi ya kuikuka Katiba.
Mafanikio mengine ambayo yametajwa na Waziri Kabudi ni pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuendelea na utoaji wa ushauri wa kisheria kwenye mikataba na makubaliano mbalimbali yanayofanywa na Wizara Idara na Taasisi za Serikali. Katika eneo hilo , hadi kufikia mwezi February, 2018 Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ilifanya uhakiki na kutoa ushauri wa mikataba 691 yenye thamani ya Shilingi 1,720,026,713,823bn/- na Dola za Kimarekani 1,0884,472,366, mikataba hii ilihusu ununuzi , ukarabati wa majengo, utoaji wa huduma za jamii na ujenzi wa barabara.
Katika uendeshaji wa kesi za jinai, Waziri wa Katiba na Sheria alieleza Kamati ya kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwamba, katika kipindi kinachoishia February 2018. Ofisi ya Taifa ya Mashtaka iliendelea na kuratibu shughuli za upelelezi wa makosa ya jinai mahakamani.Mashauri ya jinai yaliyoshughulikiwa ni pamoja na yaliyohusu wanyamapori, dawa za kulevya, uhujumu uchumi, rushwa na mauaji. Ambapo washtakiwa waliotiwa hatiani walipewa adhabu mbalimbali zikiwamo vifungo, faini na mali kutaifishwa ambapo jumla ya shilingi za kitanzania 2,169 ,983,500 zilitozwa kama faini kutoka kwa washtakiwa.
Aidha kwa upande wa mali zilizotaifishwa ni pamoja na kilogramu 24.5 za dhahabu yenye thamani ya Shilingi 2,012,357,164 na fedha za kigeni kutoka mataifa 15 zenye thamani ya shilingi 908,019,979. Mali nyingine zilizotaifishwa ni pamoja na magari matano ya kifahari aina ya Range Rover Vogue na moja aina ya Audi yaliyokamatwa katika banari ya Dare s Salaam yakisafirishwa kama nguo za mitumba.
Mali nyingine zilizotaifishwa katika kipindi hicho ni pikipiki, mifugo, mafuta na basi la abiria lililokuwa likitumika kusaifirishia meno ya tembo yanazokadiriwa kuwa na thamani ya jumla ya shilingi 3,242,787, 915.
Kwa upande wa uandishi wa Sheria, Wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, iliandaa jumla ya miswaada 15 ya sheria ambayo iliwasilishwa Bungeni na kupitishwa na kuwa sheria. Hali kadharika, iliadaa sheria ndogo na matamko mbalimbali ya serikali yapatayo 164 ambayo yalichapishwa kwenye gazeti la serikali.
Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2018/2019, Wizara inaomba takribani Shilingi 183,223,038,000bn/- zikiwamo fedha za mishahara, matumizi mengineyo na miradi ya maendeleo.
Katika kikao cha leo mafungu yaliyopitishwa na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Sheria na Katiba ni yale ya Wizara, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Wakili Mkuu na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka .
Kikao hicho cha uwasilishaji wa mpango na bajeti ya Wizara kilihudhuriwa pia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi, Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome , Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Paul Ngwembe, Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Bw. Biswalo Mganga, pamoja na wawakilishi kutoka Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria.
Taasisi ambazo zipo chini ya Wizara ya Katiba na Sheria ni Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, Tume ya Utumishi wa Mahakama, Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo na Chuo cha Uongozi wa Mahakama-Lushoto.
Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe Profesa Palamagamba Kabudi ( Mb) akiwasilisha mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara na Taasisi zake leo Dodoma, pembeni yake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk.Adelardus Kilangi
Mbunge wa Ubungo Mhe. Saeed Kubena ambayi ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria akinyosha mkono kuashiria kutaka kuuuliza jambo wakati mara baada ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Profesa Palamagamba Kabudi kuwasilisha Mpango na Makadirio ya Bajeti.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakisikiliza uwasilishwaji wa Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake leo mkoani Dodoma
Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe. Najma Gingo (kushoto) akiteta jambo na Katibu wake wakati wa uwasilishaji wa Mpango na Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria na Taasisi zake
Hivyo makala WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA
yaani makala yote WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wagonjwa-55-wa-akili-waliokuwa-na.html
0 Response to "WAGONJWA 55 WA AKILI WALIOKUWA NA MAKOSA MBALIMBALI WAACHIWA"
Post a Comment