title : Wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya Moyo .
kiungo : Wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya Moyo .
Wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya Moyo .
Na Mwandishi Maalum
19/3/2018 Jumla ya wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya siku sita inayofanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Upasuaji huo unafanywa na madaktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao wa Taasisi ya Open Heart International (OHI) ya nchini Australia.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es Salaam Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa ya damu ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya upasuaji Bashir Nyangasa alisema wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji watoto ni 15 na watu wazima 10.
Dkt. Nyangasa alisema kambi hiyo imeenda sambamba na upimaji wa magonjwa ya moyo kwa wagonjwa 65 kati ya hao watoto 35 na watu wazima 30. Wagonjwa ambao wamefanyiwa uchunguzi na hawatafanyiwa upasuaji katika kambi hiyo watafanyiwa upasuaji na madaktari wa JKCI.
“Watoto tunaowafanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo ambayo ni matundu na mishipa ya damu kutopitisha damu vizuri katika moyo na kwa watu wazima tunapandikiza mishipa ya damu kwenye moyo (CABG – Coronary Artery Bypass Grafting) na kubadilisha milango ya moyo miwili hadi mitatu iliyoziba au haifungi vizuri.
Kabla ya kuanza kwa kambi hiyo kulikuwa na mafunzo ya kiuguzi ya siku tano ya utoaji huduma bora kwa wagonjwa wa upasuaji wa moyo yalitolewa na Taasisi ya Open Heart International kwa wauguzi 30 wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete.
Hadi sasa wagonjwa wanne wameshafanyiwa upasuaji wa moyo kati ya hao watoto wawili na watu wazima wawili na hali zao zinaendelea vizuri .
Mwisho.
Hivyo makala Wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya Moyo .
yaani makala yote Wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya Moyo . Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya Moyo . mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/wagonjwa-25-wanatarajiwa-kufanyiwa.html
0 Response to "Wagonjwa 25 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wa kufungua kifua katika kambi maalum ya matibabu ya Moyo ."
Post a Comment