title : Twanga Pepeta waipania Tanga hatari
kiungo : Twanga Pepeta waipania Tanga hatari
Twanga Pepeta waipania Tanga hatari

Twanga wanapanda jukwaani ikiwa ni miezi kadhaa tangu walivyoenda katika Mkoa wa Tanga, maarufu kwa Wagosi wa Kaya, jambo linaloongeza mguso kwenye shoo zao zote za Mkoa huo kutokana na kiu kubwa ya wadau wao waliokuwa na shauku ya kuiona bendi yao hiyo ikiwa jukwaani.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Twanga Pepeta, Martin Sospeter, alisema wanamuziki wao wamejipanga imara ili kudhihirisha makali yao katika tasnia nzima ya muziki wa dansi kwa kuongozwa na Luiza Mbutu, Kalala Junior, Haji Ramadhan, Msafir Diouf na wengineo wanaotamba kwenye bendi yao.
"Hakuna ubishi kuwa bendi ya Twanga Pepeta ndio alama ya muziki wa dansi nchini, hivyo ili kuonyesha umwamba huo wa kuimba vizuri, kupiga mdundo pamoja na kushambulia jukwaa, niwaombe mashabiki waje kwa wingi Ijumaa katika Ukumbi wa Tanga Hotel, kwakuwa ndio sehemu yetu ya kutangaza makali yetu.
"Mbali na onyesho la Tanga Hotel tutakaloanza mapema kabisa mishale ya saa 1 jioni, tutaendeleza dozi zetu katika Ukumbi wa Rombo Hotel Handeni Mjini siku ya Jumamosi ya Machi 24 na Jumapili ya Machi 25 tutawapa burudani mashabiki wetu wa Korogwe Mjini katika Ukumbi wa Mamba Club, huku kote viingilio vikiwa ni sh 7,000 tu," Alisema Sospeter na kuwataka mashabiki wao waende kwa wingi ukumbini kujionea umahiri wa bendi yao kongwe nchini.
Twanga Pepeta ni miongoni mwa bendi zinazotamba hapa nchini ikiongozwa na mwanamama Asha Baraka, huku ikiweza kujikita kileleni kwa muda mrefu tangu kuanzishwa kwake, huku ikiwa na nyimbo kali kama Mwana Dar es Salaam, Mtu Pesa, Nazi Haivunji Jiwe, Marry na nyinginezo zinazotesa katika ulingo wa muziki wa dansi nchini.
Hivyo makala Twanga Pepeta waipania Tanga hatari
yaani makala yote Twanga Pepeta waipania Tanga hatari Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Twanga Pepeta waipania Tanga hatari mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/twanga-pepeta-waipania-tanga-hatari.html
0 Response to "Twanga Pepeta waipania Tanga hatari"
Post a Comment