TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO

TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO
kiungo : TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO

soma pia


TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

TUME ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS), inatarajia kuanza kampeni za kitaifa kuhamasisha wanaume kupima afya zao ,ili kujenga tabia ya kujitokeza kujua afya zao kwani ni asilimia 45 pekee ya kundi hilo walioaminika kuwa na VVU ndio waliopima kujua hali zao.
Aidha imeeleza ,kati ya watu kumi wenye maambukizi mapya kwa mwaka ,vijana wanne sawa na asilimia 40 ugundulika kupata maambukizi hayo.

Pamoja na hayo ,kati ya vijana kumi waliopata maambukizi mapya kila mwaka nane huwa vijana wa kike na wawili ni vijana wa kiume.Mkurugenzi mtendaji wa TACAIDS ,Leonard Maboko aliyaeleza hayo mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .

Alisema ,kampeni hiyo itakuwa ya miezi sita na itakuwa endelevu hadi hapo watakapohakikisha wanatokomeza ama kupunguza gonjwa hilo .Maboko alisema ,wale watakaobainika kuwa na maambukizi mapya watatakiwa kuanza tiba ya dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARVs) mapema ili kuondoa vifo vinavyotokana na virusi hivyo .

Alielezea ,wanaandaa kampeni hizo kutokana na takwimu za utafiti wa viashiria vya ukimwi ya mwaka 2016/2017 inayoonyesha idadi ya watu wanaopima na wanaogundulika kuambukizwa wanaoanza kutumia dawa ni wanawake kuliko wanaume.
Mratibu wa mtandao wa viongozi wa dini wanaoishi na virusi vya ukimwi ,(TANERELA),mchungaji Amin Sandewa pichani .(picha na Mwamvua Mwinyi)

Mkurugenzi mtendaji wa Tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi (TACAIDS ) ,Leonard Maboko akizungumza jambo ,mjini Kibaha ,Mkoani Pwani ,katika mkutano ulioandaliwa na tume hiyo ,kupitia mipango ya utekelezaji wa afua za ukimwi kwa asasi mwamvuli ya mwaka 2018/2019 .(picha na Mwamvua Mwinyi).




Hivyo makala TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO

yaani makala yote TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/tacaids-kuanza-kampeni-kuhamasisha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "TACAIDS KUANZA KAMPENI KUHAMASISHA WANAUME KUPIMA AFYA ZAO-MABOKO"

Post a Comment