title : SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI
kiungo : SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI
SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI
Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus akizungumza na
Maafisa Habari na Mawasiliano kutoka katika Halmashauri na Mikoa ya
Morogoro, Manyara, Dodoma, Kilimanjaro na Tanga yaliyofunguliwa jana
jumanne Machi 20, 2018. Mafunzo hayo ya siku nne yamendaliwa na Mradi na
Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3) kwa kushirilkiana na Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa mna Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kupitia ufadhili
wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
MAAFISA Habari na Mawasiliano katika Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini wametakiwa kuacha kufungia katika makabati na makabrasha taarifa chanya za utekelezaji wa mikakati, miradi na programu mbalimbali za Serikali na badala yake watangaze mafanikio hayo kwa umma.
Hayo yamesemwa jana (Jumanne Machi 20, 2018) Mkoani Morogoro na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Rodney Thadeus wakati wa ufunguzi wa mafunzo kuhusu mwongozo wa uandishi wa habari za tovuti kupitia Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma (PS3) unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).
Thadeus alisema Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini, hivyo ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano katika maeneo hayo watangaze mafaniko hayo badala ya kusubiri maswali na hoja mbalimbali za wananchi wakihoji katika kupata uelewa kuhusu miradi hiyo.
“Maafisa Habari, msifungie taarifa katika makabati yenu toeni taarifa kwa Umma, wananchi wanapenda kufahamu nini kinafanywa na Serikali yao hivyo jukumu la Afisa Habari ni kupiga picha kuandaa taarifa na wekeni vielelezo hivyo katika tovuti zenu ili kujibu hoja za wananchi” alisema Thadeus.
Aidha, alisema ni wajibu wa Maafisa Habari na Mawasiliano kuhakikisha kuwa wanaweza taarifa mpya kila wakati ili kuhakikisha kuwa zinakidhi mahitaji ya msingi ya wananchi ambao wamekuwa wakitumia muda mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali katika maeneo yao ya kazi.
Hivyo makala SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI
yaani makala yote SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/serikali-maafisa-habari-na-mawasiliano_21.html
0 Response to "SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI"
Post a Comment