- Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa , tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title :
kiungo :

soma pia



Pix 1 Maandamano ya wanawake yakiingia uwanja wa  Mandela Mkoani Rukwa katika kusherekea Siku ya Wanawake Duniani Mkoani hapo.
Pix 2 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akicheza muziki wa kwaya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kizwite wakati wa Maadhisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Rukwa
Pix 3 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akihutubia wanawake wa Mkoa wa Rukwa na kutoa onyo kwa Wakurugenzi wa Halmashauri  nchini  wasiotenga fedha asilimia 4 ya uwezeshaji wanawake kiuchumi wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Rukwa.
Pix 4 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Mhe. Khalfan Haule akitoa salamu za mkoa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani hapo.
 Pix 5 Mkuu wa Wilaya ya Kalembo Mhe. Julieth Binjula akitoa salamu kwa niaba ya Wanawake wa Mkoa wa Rukwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Rukwa.
Pix 6 Mwakilishi wa  Ubalozi wa Canada Bi Susan akitoa salamu za wadau wa maendeleo na wanawake kwa niaba ya wadau wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Rukwa.
Pix7 Mbunge wa Sumbawanga Mjini Mhe. Haeshi Hilary akimshukuru Waziri Ummy kwa kuwezesha kufanikisha Huduma Bora za Afya ya Mama na Mtoto katika Jimbo lake na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoani hapo.
Pix 8 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akikata utepe kuzindua Jukwaa la kuwezesha Wanawake Kiuchumi mkoani Rukwa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani Hapo.
Pix 9 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akitoa zawadi kwa mmoja wa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mtihani wa darasa la Nne katika mkoa wa Rukwa.
Pix 10 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  akitoa zawadi kwa mmoja wa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika mtihani wa Kidato cha Nne katika mkoa wa Rukwa.
Pix 11 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  akitoa zawadi ya Cheti kwa Kikundi bora cha wajasiliamali cha mfano katika mkoa wa Rukwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani hapo.
Pix 12 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu  akitoa hundi ya Millioni 10 kwa ajili ya kuwezesha vikundi vya wanawake mkoani Rukwa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  Mkoani hapo.
Na Mwandishi wetu Sumbawanga
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewaonya Wakurugenzi wote wa Halmashauri watakaokaidi agizo la Serikali la kutenga asilimia 4 kwa  ajili ya wanawake na vijana pamoja na asilimia 2 kwa ajili ya watu wenye ulemavu.
Ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mkoa wa Rukwa ambapo amepokea changamoto kutoka kwa wanawake wengi  kuhusu utoaji mdogo wa mikopo na wengine kutopata kabisa mikopo kutoka Halmashauri zao.
Mhe Ummy amewaagiza Wakurugenzi wa  Halmashuri zote nchini kutenga asimilia 4 kwa ajili ya wanawake na kutoa mikopo yenye tija itaakayoweza kuwasaidia wanawake kujikwamua kiuchumi na sio kurudi nyuma kiuchumi.
“Mikopo ya laki tatu haina tija toeni mikopo yenye tija itakayoendana na kauli mbiu ya kuelekea uchumi wa viwanda” alisema  Mhe. Ummy
Mhe. Ummy ameongeza kuwa ili kufikia azma ya Tanzania ya Viwanda basi Halmashauri hazina budi kujiwekea mikakati ya kutoa mikopo mikubwa itakayowezesha wanawake na wananchi kwa ujumla kufikia dhana hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kalembo Mhe. Julieth Binjula ameiomba Serikali kuendelea kuwawezesha wanawake kwa kuwapa elimu ya jinsi ya kutumia fedha na kuendesha miradi mbalimbali itakayo wakwamua kiuchumi.
Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Khalfan Haule amesisitiza wadau kushirikiana na Serikali pale ambapo wanaweza kuwawezesha wanawake sehemu walipo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kutoa mchango katika kuchangia kujiletea maendeleo jumuishi.
Siku ya Wanawake Duniani 2018 kilele chake ni siku ya tarehe 8 Machi, 2018 na  Kaulimbiu inayoongoza maadhimisho haya ni ‘‘KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA: TUIMARISHE USAWA WA JINSIA NA UWEZESHAJI WA WANAWAKE VIJIJINI”. Dhamira ya Wizara nikuona kila mdau mmoja mmoja anaelewa madhumuni ya kaulimbiu na kuchukua hatua kuchangia utekelezaji wa ujumbe mahususi wa kuwajumuisha wanawake wa vijijini katika maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.



Hivyo makala

yaani makala yote Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/pix-1-maandamano-ya-wanawake-yakiingia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to " "

Post a Comment