MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020
kiungo : MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

soma pia


MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

NA ELISA SHUNDA,MAFIA .


VIONGOZI wanaounda Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mafia wametakiwa kujitoa kwa nguvu,mali na rasilimali zao katika kukitumikia chama hicho na kuhakikisha kinafanya vizuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu 2020 ili CCM katika wilaya hiyo kiibuke na ushindi wa kishindo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Charangwa Selemani Makwiro wakati alipofanya ziara wilayani humo leo ambapo katika kuhakikisha vijana wa wilaya hiyo wananufaika na serikali ya Dk.John Pombe Magufuli amepata fursa ya kutembelea ofisi ya wilaya na halmashauri ambapo amekutana na uongozi na kupewa maelezo ya mnufaiko wa vijana wa Mafia katika asilimia 4% ya mikopo na miradi inayotolewa na uongozi huo kwa vijana hao.

Mwenyekiti Makwiro amewaeleza vijana hao kuwa wao ndiyo nguvu ya chama na kuwataka kusimama ngangari kama viongozi na vijana wa CCM kwa kutumia nguvu,mali,akili na rasilimali zao zote katika kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi ujao wa mwakani wa serikali za mitaa ambapo ndiyo msingi wa ushindi wa uchaguzi mkuu wa madiwani,ubunge na urais hivyo ni jukumu lao vijana kukipigania chama katika maandalizi ya uchaguzi huo.

“nimefarijika siku ya leo kukutana na viongozi na vijana wa CCM wa Wilaya hii ya Mafia napenda kuwausia na kuwakumbusha vijana wenzangu mmeomba nafasi za uongozi kwenye maeneo yenu hivyo basi unapoomba nafasi katika chama hiki usitarajie labda kuna hela utapata au uwe kibaraka wa kiongozi Fulani ili maisha yako yaendelee hapana umeomba nafasi ya uongozi kwa ajili ya kuwatumikia vijana wenzako ni jukumu lako kama kiongozi sasa kutumia nguvu zako,akili,mali na rasilimali katika kukitumikia chama hiki;

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na viongozi na wajumbe chama hicho wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani leo,Kiongozi huyo yupo katika ziara ya kutembelea jumuiya za umoja wa vijana wa Mkoa huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Mafia,Amina Tuki wengine kulia ni Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango. Picha zote na Elisa Shunda
Katibu Tawala wa Wilaya ya Mafia,Gilbert Sandagula akitoa ufafanuzi wa ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Halmashauri kwa ujumla jinsi inavyosaidia vijana wa wilaya hiyo kunufaika na mikopo na miradi mbalimbali inayotolewa na ofisi hizo kwa vijana.Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro akiulizia mambo mbalimbali yahusuyo vijana wa Wilaya ya Mafia kwa uongozi wa wilaya hiyo ofisini hapo.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Mafia,Hassan Pango,akizungumza wakati Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Seleman Makwiro na Mjumbe wa Baraza Kuu Taifa UVCCM Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao walipowasili katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mafia kupokea taarifa ya usaidizi wa ofisi hiyo katika kuwasaidia vijana wa wilaya hiyo kwenye mikopo ya asilimia 4%.




Hivyo makala MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

yaani makala yote MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mwenyekiti-uvccm-mkoa-pwani-awataka.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020"

Post a Comment