title : MKURUGENZI MKUU MSD AMTAJIA RAIS MAGUFULI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI
kiungo : MKURUGENZI MKUU MSD AMTAJIA RAIS MAGUFULI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI
MKURUGENZI MKUU MSD AMTAJIA RAIS MAGUFULI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD) Lauraean Bwanakunu pamoja na mafanikio ambayo wameyapata katika kutekeleza majukumu yao ya kununua, kusambaza, kutunza na kusambaza dawa na vifaa tiba, changamoto inayowakabili ni ya ununuzi wa vifaa vya kitaalam toka wazalishaji.
Ametaja baadhi ya vifaa hivyo ni vya macho, meno, moyo na figo ambapo vinaagizwa kwa uchache na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI),Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) na ORIC.
Azungumza leo jijini Dar es Salaam mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa magari mapya ya msaada ya kusambaza dawa ambayo yametolewa na Global Fund kwa MSD, Bwanakunu amesema wazalishaji wa vifaa hivyo wanaona oda ni ndogo na hivyo wamekuwa na wakati mgumu kupata.
Amemhakikishia Rais Magufuli kuwa, MSD wamejipanga kukabiliana na changamoto hiyo na mwezi ujao watazungumza na Shirika la IDA lililopo Denmark na wengine ili kuwakusanyia vifaa hivyo pamoja na nchi nyingine kwa lengo la kuwapunguzia gharama za manunuzi.
Amesema kampuni hizo hufanya manunuzi ya nchi mbalimbali ikiwemo umoja wa mataifa na hivyo wanataka kufaidika na mfumo huo.
Bwanakunu amemueleza Rais Magufuli , changamoto ya pili wanayokabiliana nayo ni ya maoteo kutokana na kutokuwa sahihi na kufanya suala la ununuzi kuwa la kubahatisha.
Akizungumzia kuongezeka kwa bajeti ya kununua dawa kutoka Sh.bilioni 31 hadi Sh.bilioni 250, Bwanakunu amesema yale yalikuwa maajabu na kama ndoto na kila mtu kwenye mnyororo wa ugavi alichanganyikiwa ghafla.
"Kuna zahanati ilikuwa inapata dawa za Sh.400,000 kwa mwaka na sasa inapata Sh.milioni 10. Furaha hii haikuwa kwa vituo vya kutolea huduma za afya , watumishi wa afya lakini zaidi sisi watumishi wa MSD umetuondolea kero ya Watanzania kudhani mtu akiumwa na mbwa au nyoka basi shida ni MSD wakati hatuna fedha za kununua dawa hizo.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Madawa, Laurean Bwanakunu akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 181 yatakayokuwa yakisafirisha vifaa tiba na vitendanishi katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika leo Jumatatu Machi 26, 2018 katika Ofisi za MSD Keko Mwanga Jijini Dar es Salaam.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MKURUGENZI MKUU MSD AMTAJIA RAIS MAGUFULI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI
yaani makala yote MKURUGENZI MKUU MSD AMTAJIA RAIS MAGUFULI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MKURUGENZI MKUU MSD AMTAJIA RAIS MAGUFULI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mkurugenzi-mkuu-msd-amtajia-rais.html
0 Response to "MKURUGENZI MKUU MSD AMTAJIA RAIS MAGUFULI CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI"
Post a Comment