title : MBOWE NA WENZAKE WAPELEKWA MAHABUSU
kiungo : MBOWE NA WENZAKE WAPELEKWA MAHABUSU
MBOWE NA WENZAKE WAPELEKWA MAHABUSU
*Mahakama yaamua kuwanyima dhamana kwa usalama wao
*Hatma yao kujulikana Ijumaa iwapo watatoka mahabusu au la
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
MWENYEKITI wa Chadema Freeman Mbowe na viongozi wengine wa chama hicho ambao wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wamepelekwa mahabusu baada ya upande wa Jamhuri kuwasilishwa maombi ya kuwanyima dhamana.
Mbali ya Mbowe wengine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Bara Salum Salum, Mbunge wa Kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko na Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Vicent Mashinji.
Hivyo baada ya kusikiliza mabishano marefu ya upande wa Jamuhuri na ule wa utetezi juu ya dhamana ya washtakiwa kama wapate au la, mahakama imesema itatoa uamuzi Machi 29 mwak huu, mshtakiwa Mbowe na wenzake wamepelekwa rumande.
Mapema upande wa Jamuhuri uliwasilisha mahakamani hapo maombi ya kunyimwa dhamana kwa washtakiwa kwa njia ya mdomo.
Akiwasilisha sababu za kupinga dhamana mahakamani hapo, Wakili wa Serikali Mkuu Dk.Zainabu Mango amedai ni kwasababu za usalama wa jamii na nchi kiujumla kama ilivyoelezwa kwenye hati ya mashtaka.
Amedai wanatambua dhamana ni haki ya mshtakiwa lakini hakuna haki isiyokuwa na wajibu kwa mujibu wa katiba ya nchi. Kwani Mashtaka yao wanaashiria kutokutii amri yao kikatiba, utekelezaji wa haki binafsi unapaswa kuzingatia haki za watu wengine.
Alidai makosa yanayowakabili yanahatarisha usalama nchi na kuwapa dhamana ni kuendelea kuwapa nafasi ya kuendelea kufanya makosa hayo
"Jukumu la dhamana liko chini ya mahakama hii, hata hivyo kabla ya mahakama kutumia mamlaka yake kutoa ama kuzuia dhamana inapaswa kuangalia mazingira ya kosa husika"amedai Dk.mango.
Ameiomba Mahakama kuzingatia maslahi ya umma kwa ujumla wake kwa hatari ya makosa wanayoshtakiwa nayo na usalama wa taifa.
Wakili Faraja alidai kuwa kama washtakiwa wataruhusiwa kurudi uraiani baada ya matamko hayo ni wazi kwamba haki ya upande wa pili itapotea, matamshi yaliyotolewa na washtakiwa yana madhara endelevu kwa watanzania kwani tuna taarifa za upelelezi kwamba baadhi ya mambo yaliyoongelewa, ushawishi uliotolewa unaonekana kuna utekelezaji wa kihalifu.
Akijibu hoja hizo Wakili wa utetezi Peter Kibatala amedai hakuna chochote cha kisheria kilichozungumzwa kutoka kwenye dawati, Kilichoko mbele ya mahakama sio maombi ni pingamizi la dhamana na hakuna ushahidi wowote kwa yaliyosemwa.
Pia Kibatala amedai Wakili anashindwa kutofautisha askari mpelelezi na mawakili wasomi na Mahakama haiwezi kumnyima mtu dhamana kwa taarifa ambazo haziko mahakamani.
Aliendelea kudai hati ya mashtaka haina jina wala sahihi ya aliyeandaa jambo ambalo limekatazwa na Mahakama Kuu.
Hivyo makala MBOWE NA WENZAKE WAPELEKWA MAHABUSU
yaani makala yote MBOWE NA WENZAKE WAPELEKWA MAHABUSU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MBOWE NA WENZAKE WAPELEKWA MAHABUSU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mbowe-na-wenzake-wapelekwa-mahabusu.html
0 Response to "MBOWE NA WENZAKE WAPELEKWA MAHABUSU"
Post a Comment