mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno

mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno
kiungo : mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno

soma pia


mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno

 Daktari bingwa wa meno kutoka Chuo kikuu cha AJMANI cha Falme za kiaarabu,  Zaid Mohammed Hassan akimfanyia uchunguzi wa meno mwanafunzi wa skuli ya Mwanakwerekwe H Juma Hassan katika zoezi la kutoa matibabu yaliofanyika skulini hapo.

Na Kijakazi Abdalla-MAELEZO
JAMII imetakiwa itumie mbinu sahihi ili kuimarisha afya kinywa na meno na kupunguza mzigo mkubwa wa kutibu maradhi ya meno.  

Akizungumza katika kampeni maalum juu ya kujikinga na maradhi yanayoathiri kinywa na meno katika skuli ya msingi Mwanakwerekwe ‘E’, Daktari Dhamana Kanda ya Unguja Muhidin Abdalla Mohammed, amesema wananchi wengi wamebainika kuathiriwa na maradhi ya kinywa na meno.

Kwa hivyo amesema ipo haja ya kuchukua tahadhari ili kupunguza tatizo hilo. Aidha, alisema lengo la kampeni hiyo ni kuinua uwelewa wa watu ambao hawatoi kipaumbele kwa afya ya kinywa na meno, na hivyo kujikuta wakisumbuka kuhahangaikia matibabu.

 Dkt. Muhidini Abdalla wa meno kanda ya Unguja  akiwapatia elimu fupi wanafunzi wa skuli ya Mwanakwerekwe E namna ya kusafisha meno.

Dk. Muhiddin pia amesema hatua ya kufanya kampeni hiyo katika skuli, inalenga kuwapa elimu wanafunzi juu ya namna bora na sahihi za kutunza meno na kupiga mswaki ili waimarishe afya ya meno yao.

Alisema katika umri mdogo, ndipo watoto hupitia mabadiliko makubwa kimwili, hivyo kuwapa taaluma kutawawezesha kufahamu mbinu sahihi za kuimarisha afya na kujikinga wanapokua wakubwa.

Hata hivyo, ameiomba Serikali iongeze juhudi zaidi kufikisha huduma za meno kila eneo ingawa kunahitaji gharama kubwa, lakini akasema kuacha watu waugue bila tiba ni gharama zaidi.

Alieleza kuwa, tangu kuanza kampeni hizo kuelekea maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno kimataifa, zaidi ya watoto 1,000 wametibiwa kwa kushirikiana na madaktari kutoka Ujerumani, Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE) pamoja na Wizara ya Afya.

 Daktari dhamana wa Meno kanda ya Unguja alievalia vazi jeupe Muhidini Abdalla akishirikiana na madaktari bingwa kutoka Ujerumani na Falme za Kiarabu wakimng’oa jino mwanafunzi Aisha Makame wa skuli ya Mwanakwerekwe H katika matibabu yaliofanyika skulini hapo.

Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi Mwanakwerekwe ‘E’ Khitiyar Haidhuru Ramadhani,  alisema ujio wa madaktari hao umewapa faraja  wanafunzi na elimu sahihi ya kutunza meno yao.

Aidha aliwataka wazee kujenga utamaduni wa kuwanunulia watoto vitu vinavyoweza kuwaepusha na maradhi ya meno kama vile pipi, biskuti na chokoleti ambavyo huchangia zaidi maradhi hayo.

BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


Hivyo makala mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno

yaani makala yote mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mbinu-sahihi-zatakiwa-kutumika-ili.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "mbinu sahihi zatakiwa kutumika ili kuimarisha afya kinywa na meno"

Post a Comment