title : MASHINE ZA KUTOA SUMU ZINAZOTUMIWA NA WAGANGA TIBA MBADALA ZAPIGWA MARUFUKU
kiungo : MASHINE ZA KUTOA SUMU ZINAZOTUMIWA NA WAGANGA TIBA MBADALA ZAPIGWA MARUFUKU
MASHINE ZA KUTOA SUMU ZINAZOTUMIWA NA WAGANGA TIBA MBADALA ZAPIGWA MARUFUKU
Mwamba wa habari
Serikali imepiga marufuku matumizi ya mashine zinazodaiwa kuondoa sumu mwilini na kutibu baadhi ya magonjwa maarufu kama Quantum, zinazotumiwa na waganga wa tiba asili na tiba mbadala nchini.
Marufuku hiyo imetangazwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati akizungumza na wanahabari.
Dkt. Ndugulile amesema mashine hizo zimekuwa zikiingizwa nchini bila ya kuchungunzwa na kuthibitishwa ubora wake na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, kitendo kinachohatarisha usalama wa afya ya mtumiaji.
“Marufuku kuingiza na kutumia mashine hizo zinazofahamika kwa jina la Quantum sababu hatujazipima na kuzithibitisha,” amesema.
Naye Msajili kutoka Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dkt. Ruth Suza amesema baraza hilo limeanza zoezi la kuwakamata waganga wa tiba asili na tiba mbadala wanaotumia mashine hizo.
“Hatukamati wanaotumia mashine peke yake, bali tunakamata hata wale ambao huduma zao wanazotoa zina mapungufu,” amesema.
Hivyo makala MASHINE ZA KUTOA SUMU ZINAZOTUMIWA NA WAGANGA TIBA MBADALA ZAPIGWA MARUFUKU
yaani makala yote MASHINE ZA KUTOA SUMU ZINAZOTUMIWA NA WAGANGA TIBA MBADALA ZAPIGWA MARUFUKU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MASHINE ZA KUTOA SUMU ZINAZOTUMIWA NA WAGANGA TIBA MBADALA ZAPIGWA MARUFUKU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mashine-za-kutoa-sumu-zinazotumiwa-na.html
0 Response to "MASHINE ZA KUTOA SUMU ZINAZOTUMIWA NA WAGANGA TIBA MBADALA ZAPIGWA MARUFUKU"
Post a Comment