title : MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA MUHEZA
kiungo : MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA MUHEZA
MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA MUHEZA
*Kufanyika kesho jijini Dar es Salaam, Mhandisi Tumbo aomba wananchi kuchangia ili kufanikisha ujenzi huo
Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo amewaomba wananchi wa wilaya hiyo na Watanzania kwa ujumla kuchangia ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo ambapo kesho Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harembee ya uchagiaji fedha kufanikisha ujenzi huo.
Kwa sasa Wilaya hiyo haina Hospitali ya Wilaya na wananchi wanaohitaji huduma za afya wamekuwa wakitumia hospitali teule ya Kanisa la Anglikana ambayo imeingia mkataba na Serikali na kutokana na idadi ya wananchi wa wilayani hapo hospitali hiyo imezidiwa.
Hayo yamesemwa leo na Mhandisi Tumbo wakati akizungumzia harambee ya kuchangisha fedha inayotarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.
Mhandisi Tumbo amesema kutokana na Wilaya ya Muheza kutokuwa na Hospitali ya Wilaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974, wananchi wamekuwa wakiteseka pindi wanapohitaji huduma za afya na hivyo wakaamua kuchanishana fedha ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo.
Amefafanua tayari wananchi na wadau wa maendeleo wilayani Muheza mkoani Tanga na Watanzania kwa ujumla wameanza kuchingiaa ujenzi huo na hadi kukamilika kwake zinahitajika fedha Sh.bilioni 11.1, hivyo wakati wakisubiri fedha za Serikali Kuu na zile za kwenye bajeti wameamua kuanza kwa kuchangisha fedha hizo.
"Kesho tutakuwa na harambee itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni ambapo wananchi wa Wilaya ya Muheza wanaoishi Dar es Salaam pamoja na watanzania wengine tunaomba wajitokeze kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya.
Mkuu wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo(wa kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu harambee ya uchangiaji fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya ya Muheza katika ukumbi wa Golden Tulp jijini Dar es Salaam leo.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA MUHEZA
yaani makala yote MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA MUHEZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA MUHEZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/makamu-wa-rais-mgeni-rasmi-harambee-ya.html
0 Response to "MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA HOSPITALI WILAYA YA MUHEZA"
Post a Comment