title : MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA HALIMA MDEE ALIVYOITA WAANDISHI KUPINGA KAULI YA RAIS
kiungo : MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA HALIMA MDEE ALIVYOITA WAANDISHI KUPINGA KAULI YA RAIS
MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA HALIMA MDEE ALIVYOITA WAANDISHI KUPINGA KAULI YA RAIS
Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa mbunge wa Kawe jijini Dar as Salaam, Halima Mdee aliitisha mkutano na waandishi wa habari ili kupinga kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo.
Ofisa wa Polisi, D/SSGT Arbogast ameyaeleza hayo leo,wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mfawidhi, Victoria Nongwa baada ya kutupilia mbali kielelezo cha maelezo ya onyo kilichotolewa na upande wa mashtaka.
Akisoma uamuzi uliotupilia mbali kielelezo, Hakimu Nongwa amesema ametupilia mbali kielelezo cha upande wa mashtaka kwa sababu maelezo ya onyo ya mshtakiwa yalichukuliwa nje ya muda.
Akitoa ushahidi wake Arbogast amedai yenye ndiye aliyemfanyia mahojiano Mdee ambaye alikiri kuitisha mkutano na waandishi wa habari, July 3,mwaka 2017.Amedai mshtakiwa alimwambia ni kweli aliitisha mkutano na waandishi wa habari na lengo lake lilikuwa ni kupinga kauli ya Rais John Magufuli ya kuzuia wanafunzi wanaopata ujauzito kutoendelea na masomo.
Shahidi huyo amedai Mdee katika kituoni Oysterbay, July 8, mwaka jana na wakati akimhoji alimsikilizisha CD iliyokuwa na matamshi ya lugha ya fedheha dhidi ya Rais Magufuli.Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 29, ambapo upande wa mashtaka utaendelea kuleta mashahidi.
Mdee anakabiliwa na kesi ya kutumia lugha ya fedheha kwa Rais Magufuli, ambapo alitenda kosa hilo Julai 3,mwaka 2017 katika ofisi za makao makuu ya Chadema imtaa wa Ufipa Kinondoni.
Hivyo makala MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA HALIMA MDEE ALIVYOITA WAANDISHI KUPINGA KAULI YA RAIS
yaani makala yote MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA HALIMA MDEE ALIVYOITA WAANDISHI KUPINGA KAULI YA RAIS Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA HALIMA MDEE ALIVYOITA WAANDISHI KUPINGA KAULI YA RAIS mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/mahakama-yaelezwa-namna-halima-mdee.html

0 Response to "MAHAKAMA YAELEZWA NAMNA HALIMA MDEE ALIVYOITA WAANDISHI KUPINGA KAULI YA RAIS"
Post a Comment