MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA

MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA
kiungo : MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA

soma pia


MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA

Na Mwamvua Mwinyi,Kibaha

JESHI la polisi mkoani Pwani, limetoa siku saba kwa madereva pikipiki (bodaboda) ambao walitelekeza pikipiki zao katika vituo mbalimbali vya polisi, kwenda kuzichukua baada ya kusamehewa na jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa polisi mkoani humo, (ASP) Jonathan Shanna ,alisema jeshi hilo liliwahi kuendesha zoezi la ukamataji wa pikipiki kwa makosa mbalimbali ambapo baadhi ya madereva walizitelekeza pikipiki hizo hadi sasa.

Hata hivyo alisema ,pikipiki zilizohusika kubeba bangi ,madawa ya kulevya na kutumika kufanya uhalifu hazitatolewa .Alisema wamejiwekea mikakati ya kukabiliana na ajali mwaka huu,kwa kutoa mafunzo ya sheria za usalama barabarani kwa waendesha pikipiki.

Shanna alieleza, watahakikisha wanasimamia elimu hiyo iweze kutolewa kwa madereva hao kwenye vijiwe vyao mitaani kwa kutumia askari waliopangwa kwa kila kata.Pamoja na hayo, watakuwa wanafanya operesheni za mara kwa mara ili kuwakamata wale madereva bodaboda watakaokuwa hawataki kutii sheria bila shuruti kwa kuwachukulia hatua kali na kuwafikisha mahakamani ili kupunguza ajali na vifo kwa waendesha pikipiki.

Shanna alifafanua,wanatarajia kufanya misako kwa magari aina ya Noah yanayozidisha abiria kupita kiasi na magari yanayobeba wanafunzi ambayo hayana ubora .“Tutawachukulia hatua kali na kuwafikisha mahakamani madereva na wamiliki wa magari hayo,yatakayokiuka sheria za usalama barabarani”alisema Shanna.

Shanna hakusita kutoa ushauri kwa mamlaka nyingine ikiwemo wakala wa barabara TANROADS, TARURA, kuwa waongeze juhudi katika uboreshaji wa miundombinu ya barabara kwa kuweka alama za barabarani na kuziba mashimo.


Hivyo makala MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA

yaani makala yote MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/madereva-bodaboda-waliotelekeza.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MADEREVA BODABODA WALIOTELEKEZA PIKIPIKI ZAO VITUO VYA POLISI PWANI WAZIFUATE -RPC SHANNA"

Post a Comment