title : DHAMANA YA RUGEMARILA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI
kiungo : DHAMANA YA RUGEMARILA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI
DHAMANA YA RUGEMARILA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI
Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii.
Maamuzi juu ya dhidi ya pingamizi la awali lililowasilishwa na jamuhuri katika Mahakama ya Rufaa kupinga dhidi ya maombi yaliyowasilishwa na Mfanyabiashara James Rugemarila kupinga kukataliwa kupewa dhamana Mahakama kuu kujulikana hivi karibuni.
Jopo la majaji linaloongozwa na mwenyekiti, Bernad Luanda,Batueli MMimilla na Gerald Ndika limesema litatoa uamuzi tarehe itakayopangwa na pande zote mbili zitajulishwa.Katika maombi hàyo, upande wa jamuhuri unawakilishwa na Zainabu Mango,Peter Maugo na Tumain Kweka ambapo Rugemarila alijiwakilisha mwenyewe.
Katika maombi hayo Rugemarila anaiomba mahakama ya rufaa imruhusu kufanya mabadiliko ya taarifa ya kusudio la kukata rufaa.Pia anaomba kumuunganisha mshtakiwa mwenzake katika kesi ya Economic, Harbinder Seth kama mtu muhimu katika maombi hayo na kwamba anaomba wapatiwe dhamana wakati rufaa yao inaendelea kusikilizwa.
Upande wa jamuhuri uliwasilisha pingamizi la awali na kupinga maombi hayo kwa madai yameletwa chini ya kifungu kisicho sahihi kwani hakielekezi maombi hayo ni ya jinai au madai na kuiomba mahakama iyatupilie mbali
baada ya kusikiliza pingamizi hilo mahakama imesema itawataarifu wahusika tarehe ya kutolewa kwa uamuzi huo.Baada ya kusema hayo Rugemarila aliiomba mahakama itupilie mbali pingamizi la jamuhuri kwasababu pingamizi hilo limeletwa kwa kanuni isiyo sahihi.
Alidai pingamizi hilo halina ufafanuzi kuhusu sababu za pingamizi na kuiomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo na ataeleza kwanini amemuunganisha Seth kama mtu muhimu.
Washtakiwa wote kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi, utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya Dola za kimarekani 22, 198,544.60 na Sh, bilion 309
Hivyo makala DHAMANA YA RUGEMARILA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI
yaani makala yote DHAMANA YA RUGEMARILA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DHAMANA YA RUGEMARILA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/dhamana-ya-rugemarila-kujulikana-hivi.html
0 Response to "DHAMANA YA RUGEMARILA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI"
Post a Comment