HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI

HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI
kiungo : HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI

soma pia


HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI

 Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akikabidhi Msaada wa Vitanda 4o na Magodoro 40 kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe kwaajili ya hospitali ya mwananyamala jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusheherekea siku ya Mwanamke duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8. Benki hii imetoa vitanda na magodoro kwaajili ya wodi ya akina mama katika hospitali hiyo.
 Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda 40 na magodoro 40 katika hospitali ya Mwananyamarla jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe na kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe akishukuru kwa Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda  kwa kuiona hospitali ya Mwananyamala kwa kuwa kunahospitali nyingi"Tunashukuru Mchango wenu sana Mungu awabariki ."
kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda na Kulia ni Mkuu wa matawi ya Kanda Elizabeth Mayengo.

BENKI  ya Exim Tanzania leo imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa Mwananyamala, jijini Dar es Salaamkwa kuwa Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika hospitali ya Mwananyamala wakiongozwa na wafanyakazi wanawake wa Benki ya Exim kwenye hospitali hiyo jengo la utawala  katika hospitali hiyo ukipokelewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala Dk. Khadija Shebe.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Matawi ya benki ya Exim, Agnes Kaganda amesema “Katika kuadhimisha sherehe za wanawake mwezi huu, Benki ya Exim inatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii na kwenye ukuaji wa uchumi. Msingi wa mpango wetu huu wa mwaka mzima wa kujali jamii ni kuelewa kiasi gani wanawake ni muhimu katika jamii".

Benki imejitolea kusherehekea maadhimisho ya miaka 20 kwa kusaidia wanawake kwa kuboresha huduma za uzazi katika sekta ya afya. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa ya kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu na sisi tumejizatiti kwenye mpango huu."

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya kwa wanawake nchini. Aliongezea kwa kusema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii .”


Hivyo makala HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI

yaani makala yote HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/hospitali-ya-mwanyamala-yanufaika-na.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "HOSPITALI YA MWANYAMALA YANUFAIKA NA MSAADA WA EXIM BENKI"

Post a Comment