GATI YA LINDI YAKAMILIKA

GATI YA LINDI YAKAMILIKA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa GATI YA LINDI YAKAMILIKA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : GATI YA LINDI YAKAMILIKA
kiungo : GATI YA LINDI YAKAMILIKA

soma pia


GATI YA LINDI YAKAMILIKA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA) kwa kukamilisha ujenzi wa gati ya Lindi na kuwataka kutafuta masoko ili bandari hiyo iweze kunufaisha Serikali na wananchi wa Mkoa huo. 

Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa gati hiyo mkoani Lindi ambapo amesema mradi umekamilika kwa asilimia 92 na kukamilika kwa gati hiyo kutarahisisha biashara na kukuza uchumi kwa wananchi kwani meli kubwa zitaanza kutia nanga katika bandari hiyo. 

“Napenda kuwapongeza sana TPA kwa kazi kubwa mliyoifanya kukamilisha mradi huu, ni wakati sasa mkatafute masoko ili mpate faida na kurahisisha usafirishaji kati ya mkoa huu na visiwa vinavyozunguka” amesema Prof. Mbarawa. 

Waziri Prof. Mbarawa ameongeza kuwa pamoja na kukamilisha mradi huo TPA itunze miundombinu hiyo na kuifanyia ukarabati wa mara kwa mara ili iweze kudumu kwa muda mrefu. 

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Karim Mattaka, amemuhakikishia Waziri Prof. Mbarawa, kuwa Mamlaka itazingatia maelekezo yake na kuahidi kusimamia sehemu ndogo iliyobaki ili iweze kukamilika kwa wakati na viwango vilivyokubaliwa. 
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA, Eng Karim Mattaka, akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kulia), kuhusu hatua za ujenzi wa gati ya Lindi, wakati Waziri huyo alipotembelea mradi kukagua maendeleo yake.
 Muonekano wa Gati mpya ya Bandari ya Lindi ambayo ujenzi wake umekamilika kwa asilimia zaidi ya  90. Gati hiyo imegharimu kiasi zaidi ya shilingi bilioni 3 ikiwa ni fedha za Serikali kwa asilimia 100.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akipanda kwenye boti kuelelekea katika eneo la Kitunda mkoani Lindi, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho ya kivuko Mkoani humo. Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wakazi wa Mkoani humo kuwa kivuko hicho kitawasili na kuanza kutoa huduma mwishoni mwa wiki hii.
 Muonekano wa hatua ilipofikia Gati ya kuegeshea kivuko katika eneo la Kitunda Mkoani Lindi. Ujenzi wa Gati hiyo umefikia asilimia zaidi ya 90 na imejengwa kwa fedha za Serikali.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akishiriki katika kuchanganya zege katika ujenzi wa barabara ya maegesho ya kivuko Mkoani Lindi, alipokagua maendeleo ya ujenzi wake.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa akiongea na wakazi wa Mkoani Lindi, mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi maegesho ya Kivuko. Waziri Prof. Mbarawa amewahakikishia wakazi hao kuwa kivuko kitawasili katikatia ya wiki na kuanza kazi mwishoni mwa wiki.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala GATI YA LINDI YAKAMILIKA

yaani makala yote GATI YA LINDI YAKAMILIKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala GATI YA LINDI YAKAMILIKA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/gati-ya-lindi-yakamilika.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "GATI YA LINDI YAKAMILIKA"

Post a Comment