title : DC SOPHIA MJEMA AZINDUA UPANDAJI MITI, APIGA MARUFUKU WANAOPIKA BARABARANI
kiungo : DC SOPHIA MJEMA AZINDUA UPANDAJI MITI, APIGA MARUFUKU WANAOPIKA BARABARANI
DC SOPHIA MJEMA AZINDUA UPANDAJI MITI, APIGA MARUFUKU WANAOPIKA BARABARANI
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema akipanda mti kuashiria uzinduzi wa wiki ya upandaji Miti katika wiaya hiyo.
Na Heri Shaaban
WILAYA ya Ilala jijini Dar es Salaam wazindua wiki ya upandaji miti katika wilaya hiyo ambapo mwaka huu wamepanga kupanda miti milioni 1.5.
Akizungumza leo Dar as Salaam wakati wa kuzindua kampeni hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema katika kukabiliana na tabia ya nchi na kuboresha mandhari wameendeleza kampeni endelevu ya upandaji miti kama ( Mti Wangu)ambayo ilizinduliwa mwaka Jana na Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaaam Poul Makonda.
" Katika Wilaya yangu ya Ilala tumezindua wiki ya upandaji miti na utunzaji wa miti ni mpango shirikishi ambapo manispaa yetu inashirikiana na wadau wa mazingira kupanda na kutunza miti katika msimu wa jua na mvua," amesema Mjema.
Ameongeza kampeni hiyo kila mti utakuwa na mmiliki wake hiyo maana halisi ya mti Wangu na kwamba miti ina faida nyingi kwa jamij yetu ikiwemo kutupatia matunda,kivuli, dawa za asili, mapambo ,kuzuia mmonyoko wa ardhi , hewa safi, kupunguza hewa ya ukaa na kuleta mvua.
Pia miti husaidia kupatikana mkaa na mbao. Aidha amesema misitu yetu inahifadhi wanyama pori ambao ni kivutio kwa watalii na kuipatia nchi yetu fedha za kigeni.
Amesema kila mwananchi wa wilaya ya Ilala hana budi kuthamini uwepo wa mti katika mazingira yake na uzinduzi huo unakwenda sambamba na upandaji miti katika fukwe, zahanati, hospitali , Shule za msingi na Sekondari kwenye kata na mitaa.
Ametoa mwito kila mwananchi aliopo wilayani Ilala kupanda miti katika maeneo yanayowazunguka na viongozi wa halmashauri kuhakikisha miti wanapanda na ina kua ili mchakato huo uwe na tija.
Ameziagiza halmashauri kuwa na vitalu vya miti kwa ajili ya kupunguza gharama kubwa kununua miche kila mwaka pia waeshimu kauli mbiu ya mwaka huu (Tanzania ya kijani inawezekana panda mti kwa Maendeleo ya viwanda.).
Amepiga marufuku kupika barabarani ,chakula wananchi kukatisha sehemu zilizopandwa miti , na kutema mate hovyo.
Kwa upande wake Diwani ya Chanika (CCM) Ojambi Masaburi amesema kata ya Chanika ina wakazi 40,000 na ameagiza wananchi wake kila kaya kupanda miti mitano mpaka kufikia siku ya kilele miti 100,000 iwe imeshapandwa.
Masaburi amesema wanaunga na Mkuu wa Wilaya katika kutekeleza agizo la Serikali kama sehemu ya utekelezaji wa Ilani .
Mwaka Jana alipanda miti 29,000 na mwaka huu anatarajia kuvuka lengo kupanda miti zaidi ya mwaka jana.
Hivyo makala DC SOPHIA MJEMA AZINDUA UPANDAJI MITI, APIGA MARUFUKU WANAOPIKA BARABARANI
yaani makala yote DC SOPHIA MJEMA AZINDUA UPANDAJI MITI, APIGA MARUFUKU WANAOPIKA BARABARANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC SOPHIA MJEMA AZINDUA UPANDAJI MITI, APIGA MARUFUKU WANAOPIKA BARABARANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/dc-sophia-mjema-azindua-upandaji-miti.html
0 Response to "DC SOPHIA MJEMA AZINDUA UPANDAJI MITI, APIGA MARUFUKU WANAOPIKA BARABARANI"
Post a Comment