Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho

Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho
kiungo : Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho

soma pia


Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho

 Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) Hassan Juma Amuor akizungumza na Waandishi wa habari kuhusu mabadiliko ya bei za mafuta .
Waandishi wa habari  wakiwa katika mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (ZURA) huko Maisara Zanzibar kuhusu mabadiliko ya  bei mpya za mafuta  (Picha na Kijakazi Abdalla Maelezo)


Na Kijakazi Abdalla                   Maelezo    
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya ya mafuta ambayo itaanza kutumika kesho Jumanne 13/03/2018.
Akizungumza na Waandishi wa habari Afisa Uhusiano wa  Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati(ZURA) Hassan Juma Amuor amesema kuwa  Zura imetangaza bei  mpya kwa kuzingatia mambo yafuatayo.
Alisema kuwa wastani wa mwenendo wa mabadiliko ya bei za mafuta duniani,thamani ya shilingi ,gharama za usafiri ,kodi za Serikali pamoja na kiwango cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.
Aidha alisema kuwa bei hizo Petroli kwa mwezi wa Machi 2018 imepanda kwa shilingi moja(1)kwa lita kutoka shilingi 2,256 hadi kuwa shilingi 2,257 sawa na ongezeko la asilimia 0.04%.
Bei ya mafuta ya Dizeli kwa mwezi wa Machi .2018 imepanda kwa shilingi(68)kwa lita kutoka shilingi 2,175 hadi kuwa shilingi 2,243 sawa na asilimia 3%.
Pia Afisa Uhusiano huyo alisema  bei ya Mafuta ya taa kwa mwezi wa Machi.2018 imepanda kwa shilingi (5) kwa lita kutoka shilingi 1,641 hadi shilingi 1,646 sawa na ongezeko la asilimia 0.3%.
Vilevile alisema kuwa bei ya mafuta ya Banka kwa mwezi wa Machi 2018 imepanda kwa shilingi (68) kwa lita kutoka shilingi 2,017 hadi shilingi 2,085 sawa na ongezeko la asilimia 3%.
Hata hivyo alisema kuwa bei ya Mafuta ya Ndege (Jet A-1) kwa mwezi wa Machi 2018 imeshuka kwa shilingi 4.46 kwa lita kutoka shilingi 1,811.80 hadi shilingi 1,807.34 sawa na upungufu wa asilimia 0.24%.


Hivyo makala Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho

yaani makala yote Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/bei-mpya-za-mafuta-kuanza-kutumika-kesho.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Bei mpya za mafuta kuanza kutumika kesho"

Post a Comment