title : AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO
kiungo : AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO
AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO
Picha ya Pamoja mara baada ya kuzindua duka Wilayani Gairo.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe(Kulia) akilishwa keki wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Airtel Wilayani Gairo.
HATIMAYE Kampuni ya Simu ya Airtel yawatendea haki wana Gairo.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Airtel.
Kwa kiasi kikubwa mtandao wa Airtel ndio mkombozi mkubwa wa wananchi wa Gairo hasa vijijini. Bado mawasiliano ya simu ni changamoto kubwa sana Gairo.
Mhe. Mchembe aliendelea kuwapongeza Airtel kwa ajira zaidi ya 400 nchini kupitia ofisi zinazozinduliwa sasa. Vijana wa Gairo pia ni wafaidika wa Ofisi hizo.
Kabla ya kufunguliwa ofisi hizo, wananchi walikuwa wanaenda Dodoma au Morogoro kwa huduma mbalimbali zinazohitaji kushughulikiwa na Airtel wenyewe.
Mhe. Mchembe anayakaribisha mashirika mengine ya simu kufungua ofisi Gairo. Wilaya inakuwa kwa kasi kubwa na mzunguko wa pesa ni mkubwa na mawasiliano yanahitajika kwa kasi kubwa.
Hivyo makala AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO
yaani makala yote AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/03/airtel-yafungua-ofisi-wilaya-ya-gairo.html
0 Response to "AIRTEL YAFUNGUA OFISI WILAYA YA GAIRO"
Post a Comment