title : WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU
kiungo : WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU
WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii irudi kwenye maeneo yote yenye migogoro ya mipaka na iungane na Halmashauri za wilaya ili waweze kutoa majibu kwa wananchi.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Februari 8, 2018) wakati akijibu swali la mbunge wa Urambo, Bibi Margaret Sitta wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu Bungeni mjini Dodoma.
Bibi Sitta alitaka kujua Serikali imeweka taratibu na mikakati gani ya kumaliza migogoro ya mipaka inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya hifadhi za misitu nchini kwa kuwa wananchi wanahitaji maeneo kwa ajili ya shughuli za kilimo na mifugo.
Waziri Mkuu amesema Serikali iliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii iweke vigingi kwenye maeneo yote yanayozunguka hifadhi za misitu ili kuweka alama zitakazopunguza migogoro ya kuingiliana kati ya wananchi walioko kwenye vijiji na wahifadhi kwenye maeneo ya hifadhi ya misitu hiyo.
Amesema maagizo hayo yalitolewa baada ya kugundua kuwa kuna migogoro mingi kati ya wananchi walioko katika vijiji vya jirani na misitu iliyohifadhiwa kisheria ambayo ina ramani.
“Lakini tunatambua kwamba wanapoendelea na zoezi hilo la uwekaji alama, inaweza kutokea kijiji kikajikuta kipo ndani ya mipaka ya hifadhi na inaweza kusababisha kutoelewana kati ya wanakijiji na wenye mamlaka ya hifadhi.”
Hivyo makala WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU
yaani makala yote WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/wizara-ya-maliasili-yaagizwa-irudi-kwa.html
0 Response to "WIZARA YA MALIASILI YAAGIZWA IRUDI KWA WANANCHI KUTOA MAJIBU"
Post a Comment