Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa

Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa
kiungo : Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa

soma pia


Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Sumbwanga Dk. Khalfan Haule kuhakikisha anatafuta dawa ya kuulia panya wakiwa mashambani ili kuokoa miti kutokana na uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya.

Amesema kuwa ameisikia changamoto hiyo ya uchomaji wa misitu kwasababu ya uwindaji wa panya kutoka kwa vijana mbalimbali wanaojishughulisha na mashamba ya upandaji miti pamoja na taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga juu ya changamoto za kuendeleza misitu.

“DC tafuta dawa ya panya, wauliwe huko mashambani, ili panya wasiwepo na miti iokoke, mbona hamshangilii? Hawa panya tutawaua kwa sumu huko mashambani wasiwe chanzo cha mioto ambayo mnachoma huko kuwatafuta hawa panya ili wafie huko huko mashimoni msiwapate,” Alisisitiza.

Agizo hilo amelitoa katika muendelezo wa kampeni ya upandaji miti mijini na vijijini katika Kijiji cha Mpwapwa, kata ya Mpwapwa, Wilayani Sumbwanga baada ya kuwauliza wananchi wa Kijiji hicho juu ya changamoto aliyoisikia ya uchomaji wa moto misitu kutokana na kuwinda panya, japo wananchi walikataa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akipanda mti katika shule ya msingi Mpwapwa, kata ya Mpwapwa Wilayani Sumbawanga ikiwa ni kampeni ya kufikisha miti Milioni 6 kwa Mkoa kwa mwaka 2017/2018.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dk. Khalfan Haule akisaidiana na mwanafunzi wa darasa la kwanza Shule ya Msingi Mpwapwa Joanita Mwanandenje kupanda mti ili kuwahamasisha wanafunzi kuwa na utamaduni wa kupanda miti na kufikisha miti milioni 3 kwa Wilaya ya Sumbawanga.
Mjumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa ACP George Kyando akijiandaa kuapanda mti katika Shule ya Msingi Mpwapwa ikiwa ni kampeni ya Mkoa kufikisha miti milioni 6 na kuhifadhi mazingira ya Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akikabidhi miche kwa Didas Kosam M/kiti wa kitongoji cha Katupa, Kijiji cha Mpwapwa chenye vitongoji vinne. Ambapo kila kitongoji kilipewa miche 200.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa

yaani makala yote Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/wawindaji-wa-panya-rukwa-kukomeshwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Wawindaji wa Panya Rukwa Kukomeshwa"

Post a Comment