Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando

Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando
kiungo : Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando

soma pia


Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando

Zaidi ya wananchi 1200 wa kata ya Kirando inayojumuisha vijiji vinne vya Mtakuja, Mpata, Kichangani na Kamwanda, Wilayani nkasi Mkoani Rukwa, wajitokeza katika kuhakikisha uchimbaji na uwekaji wa msingi wa kituo cha afya cha kirando unakamilika ili kuweza kuanza upanuzi na ujenzi wa kituo hicho kitakachohudumia kata zaidi ya nne katika tarafa ya Kirando.  

Wananchi hao wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono juhudi za Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kuhakikisha huduma hizo za kiafya zinasogezwa karibu na wananchi yao ili kuokoa maisha ya kina mama wajawazito, watoto na wahitaji wengine wa huduma hizo ambao wanaishi karibu na kituo hicho na kuongeza kuwa umbali wa kutoka Kirando hadi hospitali ya Wilaya iliyopo Namanyere ni Kilometa 61.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo aliyeongoza harambee hiyo amesema kuwa wameamua kuungana na wananchi pamoja na kuwashirikisha ili kuwajulisha wananchi juhudi zinazofanya na wananchi na kuonyesha mshikamano kuwa maendeleo hayaji bila ya mshikamano.

“Kila mtu anaguswa na afya, mtoto, mzee na kijana wote, serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli imeamua kuboresha na kupanua vituo vya afya ili huduma zisogee karibu kuliko kutegemea hospitali za wilaya, kwa hali hiyo ndio maana serikali inapanua vituo vya afya ili tuupunguze msongamano wa wagonjwa kwenye hospitali zetu pamoja na kwenye vijiji na tarafa huduma ziwe bora zaidi.” Alifafanua.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akiongea na kinamama walioshiriki kwenye Songambele ya Ujenzi wa upanuzi wa kituo cha Afya Kirando muda mfupi kabla ya kinamama hao kuruhusiwa na kuwaachia wanaume kuendelea na kazi.
  Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili kutoka kushoto) akipokezana na wananchi mawe ya msingi yanayojengewa msingi wa kituo cha afya cha kirando siku ya uzinduzi wa songambele ya upanuzi wa ujenzi wa kituo hicho.
 Wanananchi wa Kirando waliojitokeza kushiriki katika Songambele ya ujenzi wa Kituo cha afya Kirando. 

 Wanananchi wa Kirando waliojitokeza kushiriki katika Songambele ya ujenzi wa Kituo cha afya Kirando.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando

yaani makala yote Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/wananchi-zaidi-ya-1200-wajitokeza.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Wananchi zaidi ya 1200 wajitokeza Songamebele zinduzi wa Ujenzi kituo cha afya Kirando"

Post a Comment