WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23

WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23 - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23
kiungo : WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23

soma pia


WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.

WAKURUGNZI Watendaji saba wa kampuni tano za jijini Dar es Salaam wanatarajia kupanda kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 23 na Machi 12, mwaka huu.

Imeelezwa Wakurugenzi hao ambao walitakiwa kusomewa mashtaka yao leo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi ni, lakini ilishindikana kwa kuwa hawakuwepo ni Omari Mgwaya na Nelson Rubagumisa wa kampuni ya Panacom Solution Co.Ltd, Issa Lupigila wa kampuni ya Upame Co.Ltd na  Osca Chongola wa kampuni ya Nolc Engineering Company, 

Wengine ni,Petronia Mrosso na Fritz Masanjo wa Kampuni ya Skyscape International Co.Ltd, na Josephat Mwita wa kampuni ya Tan Geo Info Consult,

Washtakiwa  hao wanakabiliwa na kesi za jinai namba 38, 31, 37, 39 na 32 zote za mwaka 2018, 

Katika kesi inayomkabili Osca, Wakili wa Serikali Dereck Mukabatunzi alidai kesi ilipangwa kwa ajili ya mshtakiwa hiyo kusomewa mashtaka yanayomkabili.

Wakili wa mshtakiwa,Hassan Kihangio aliieleza mahakama kuwa mteja wake ni mgonjwa, anamatatizo katika pingili za uti wa mgongo, yupo hospitali amepewa mapumziko akaomba apangiwe tarehe nyingine ili afike asomewe mashtaka.

Kutokana na suala la ugonjwa upande wa mashtaka haukuwa na pingamizi na Hakimu Nongwa amahirisha kesi hiyo hadi Machi 12, 2018.

Naye Wakili wa Serikali Emmil Kilia aliyetakiwa kumsomea mashtaka Issa Lupagila alidai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya mshtakiwa huyo kusomewa mashtaka yanayomkabili lakini hawakuweza kumpata ili wampatie wito wa mahakama afike mahakamani hivyo wakaomba hati nyingine ya mwito.

Kilia amedai wanaendelea kumtafuta baada ya kueleza hayo Hakimu Nongwa aliamuru wapewe hati ya wito na kesi imeahirishwa hadi Machi 12,2018 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama atakuwa amepatikana ama la.

Katika kesi inayomkabili Joseph Mwita, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benson Mangowi alieleza mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo hawajaweza kumpata hivyo aliiomba mahakama itoe hati ya wito ili waweze kumpata na kumsomea mashtaka yanayomkabili.

Kesi imeahirishwa hadi Machi 12,mwaka 2018.

Katika kesi inayomkabili Omari Mgwaya na Nelson Rubagumisa, Wakili wa Serikali,Emma Msofe aliieleza Mahakama  washtakiwa hao hawajaweza kuwapata ili kuwapatia hati ya wito wa mahakama.

Hivyo aliiomba wapatie hati ya mwito nyingine ili waweze kuwapatia washtakiwa hao wafike mahakamani kusomewa mashtaka yanayowakabili.Kesi imeahirishwa hadi Machi 12,mwaka 2018.

Katika kesi inayowakabili, Petronia Mrosso na Fritz Masanjo, Wakili was Serikali, Dereck Mukabatunzi alieleza washtakiwa walipokea hati ya mwito wa mahakama ila wapo nje ya mkoa wa Dar es Salaam.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 23, mwaka 2018 ambapo washtakiwa hao watasomewa mashtaka yanayowakabili.


Hivyo makala WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23

yaani makala yote WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/wakurugenzi-saba-kufikishwa-kortini.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "WAKURUGENZI SABA KUFIKISHWA KORTINI FEBRUARI 23"

Post a Comment