title : TAARIFA YA KUSITISHA MATUMIZI YA ADA MPYA KWA WAANDAAJI WA MBIO ZA MARATHON
kiungo : TAARIFA YA KUSITISHA MATUMIZI YA ADA MPYA KWA WAANDAAJI WA MBIO ZA MARATHON
TAARIFA YA KUSITISHA MATUMIZI YA ADA MPYA KWA WAANDAAJI WA MBIO ZA MARATHON

BMT imeagiza kusitishwa ada hizo hadi Machi 5 itakapotoa maelekezo mengine baada ya kukutana na RT na waandaaji.
Sisi RT tumefedheheshwa na uamuzi huo na jinsi njia iliyotumiwa na BMT katika kulishughulikia tatizo linalodaiwa kuwa malalamiko ya waandaaji wa marathon kudai kuwa tozo hizo ni kubwa, tofauti na wanachokiandaa au kukifanya.
Kwani tuliamini, kutokana na miongozo ya kiutendaji, BMT ingekuwa mstari wa kwanza kulinda matakwa ya Katiba ya RT kiutendaji.
Tuliamini BMT inajua mamlaka ya utendaji ya RT, hivyo kabla ya kufikia uamuzi huo, ingetuita RT kwanza na kujadili hicho kinachodaiwa kuwa malalamiko, ndipo ingefikia kuanza kuchukua hatua.
KUPANDISHWA ADA;
Kutokana na mwenendo usioridhisha kwa muda mrefu kuhusu uandaaji wa mbio za Marathon kiholela, ambao ulikuwa haufuati taratibu zinazotakiwa, hata BMT yenyewe ni shahidi kutokana na matamshi mbalimbali ya Watendaji wake, RT iliamua kuchukua hatua kwa mujibu wa Katiba yake kama msimamizi mkuu wa mchezo wa Riadha nchini.
Mnamo Septemba 16, 2017 RT ilitoa mwito kwa waandaaji wa mbio za Marathon na kukutana katika moja ya kumbi za Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambako takribani waandaaji 28 - 30 walijitokeza.
Katika kikao hicho ambacho kilikuwa cha wazi na huru, RT iliwaeleza waandaaji kuhusiana na utaratibu mzima wa uandaaji wa mbio za Marathon na utaratibu mpya unaotakiwa kuanza kutumika kuanzia January 2018, ikiwamo kujisajili na kuzitenga mbio hizo katika makundi manne ya A, B, C na D kulingana na ukubwa wa mbio husika na kila kundi na gharama zake.
Hivyo makala TAARIFA YA KUSITISHA MATUMIZI YA ADA MPYA KWA WAANDAAJI WA MBIO ZA MARATHON
yaani makala yote TAARIFA YA KUSITISHA MATUMIZI YA ADA MPYA KWA WAANDAAJI WA MBIO ZA MARATHON Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TAARIFA YA KUSITISHA MATUMIZI YA ADA MPYA KWA WAANDAAJI WA MBIO ZA MARATHON mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/taarifa-ya-kusitisha-matumizi-ya-ada.html
0 Response to "TAARIFA YA KUSITISHA MATUMIZI YA ADA MPYA KWA WAANDAAJI WA MBIO ZA MARATHON"
Post a Comment