Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa

Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa
kiungo : Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa

soma pia


Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa

Na Ali Issa, MAELEZO-ZANZIBAR.13 FEBUARI, 2018
WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi leo wameupitisha mswada mpya wa sheria ya adhabu kwa makosa ya jinai.
Sheria hiyo mpya ya mwaka 2018, inafuta sheria ya adhabu kwa makosa ya jinai ya mwaka 2004.
Akisoma sheria hiyo mpya mbele ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Waziri wa Nchi (OR) Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman, alisema mswada huo umepitishwa kutokana na kuongezeka makosa ya jinai ambayo  sheria zake hazilingani na adhabu zinazotolewa kwa sasa.
Alieleza kuwa, ujio wa sheria hiyo mpya, kutatoa nafasi ya mahakimu kutoa adhabu zinazolingana na uzito wa makosa husika.
Aidha alisema sheria hiyo itafanya kazi mara baada ya kusainiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein.
Kwa upande wake, Mwanasheria Mkuu wa serikali Said Hassan Said, alisema kwa mujibu wa sheria hiyo, ni Jaji Mkuu pekee ndiye mwenye uwezo wa kutoa dhamana kwa mshtakiwa wa  makosa ambayo kimsingi hayastahiki dhamana.
Aliyataja baadhi ya makosa yasiyokuwa na dhamana kuwa ni pamoja na ubakaji, kulawiti, kuua, uhaini, kuingiza nchini na kusambaza dawa za kulevya na mengineyo.
Mwanasheria Mkuu alieleza kuwa sheria hiyo ilijadiliwa kwa umakini mkubwa na wajumbe wamejiridhisha na kuipitisha wakiamini itapunguza kilio cha wananchi kwa kutoa hukumu za haki kwa watuhumiwa wa makosa ya jinai.
Kwa upande mwengine, Naibu Waziri wa Wizara hiyo Khamis Juma Maalim alisema adhabu ya kunyongwa itaendelea kuwepo kutokana na uzito wa makosa yatakayobainika kuwa washtakiwa wanastahiki hukumu hiyo.
Aidha alisema serikali itaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili waielewe vyema sheria hiyo mpya itayo tumika mahakamani huku akiwasisitiza juu ya umuhimu wa kufuata sheria bila shuruti. 


Hivyo makala Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa

yaani makala yote Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/sheria-mpya-adhabu-ya-makosa-ya-jinai.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Sheria mpya adhabu ya makosa ya jinai Zanzibar yapitishwa"

Post a Comment