PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI

PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI
kiungo : PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI

soma pia


PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amewataka makandarasi wazawa wa kampuni ya Samota, Anam na Jossam JV wanaojenga barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 kwa kiwango cha lami wahakikishe wanakamilisha ujenzi wa barabara hiyo kwa muda uliowekwa.

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo katika kijiji cha Motomoto, Wilaya ya Urambo mkoani Tabora alipokuwa katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mtandao wa barabara mkoani humo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo.

“Nataka nione kazi za ujenzi zinafanyika kwa haraka, kwani uzoefu unaonesha baadhi ya makandarasi wazawa wamekuwa na kasi ndogo, hivyo mjipange vizuri ili barabara ikamilike kwa wakati”, amesema Prof. Mbarawa.

Amesema kuwa nia ya Serikali ni kuwajengea makandarasi wazawa uwezo ili waweze kutekeleza miradi mikubwa mingine ya ujenzi hapa nchini lakini haitasita kuwanyima kazi hizo kama miradi hiyo itacheleweshwa, haitakidhi viwango vinavyohitajika na kama hawataonekana eneo la kazi kwa kipindi kirefu.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na uongozi wa Wilaya ya Urambo, alipokutana nao katika ziara yake ya kikazi ya kukagua mradi wa ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Tabora.
 Mbunge wa jimbo la Urambo, Mhe. Magreth Sitta, akimshukuru Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (kulia), kwa kufuatilia maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 inayojengwa kwa kiwago cha lami, mkoani Tabora.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu hatua za mradi wa ujenzi wa barabara ya Urambo-Kaliua yenye urefu wa KM 28 na kusisitiza nia ya Serikali ya kuwajengea uwezo wakandarasi wazawa ili waweze kutekeleza miradi ya ujenzi hapa nchini.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, na uongozi wa wilaya ya Tabora wakipita juu ya daraja la Wala lenye urefu wa mita 34 katika barabara ya Tabora-Pangale yenye urefu wa KM 30, katika ukaguzi wa ujenzi wa barabara hiyo, mkoani humo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI

yaani makala yote PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/prof-mbarawa-awataka-makandarasi-wazawa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "PROF. MBARAWA AWATAKA MAKANDARASI WAZAWA KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI KWA WAKATI"

Post a Comment