MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO

MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO
kiungo : MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO

soma pia


MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO

WADAU wa mradi wa kuwawezesha mabinti na wanawake vijana katika sekta ya elimu wamekutana katikati ya wiki kujadili mpango kazi wa utekelezaji wa mradi wa UNESCO kwa kushirikiana na UNWomen pamoja na UNFPA unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Korea (KOICA). 

Mradi huo ambao umelenga kuondoa vikwazo vya elimu kwa wasichana na wanawake kwa kuangalia sera, sheria na kanuni zinazowezesha maendeleo kwa wanawake kwa kuzingatia matakwa ya Umoja wa Mataifa na makubaliano ya kimataifa ambayo Tanzania imetia saini ulianza mwaka 2016. 

Mradi huo unaotarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kwa kusimamiwa na Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Shirika la Wanawake la Umoja wa Mataifa (UN Women) na Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya Watu ( UNFPA) unatarajia kuiwezesha Tanzania kuwezesha elimu kwa kutumia mbinu mtambuka kwa kutambua watu wa pembezoni. Kaimu Mkuu wa ofisi na Mkuu wa kitengo cha Elimu ofisi ya Unesco Dar es Salaam, Faith Shayo akitoa neno la utangulizi wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman.

Mradi huo unatarajiwa kuwawezesha wasichana na wanawake vijana kuwa na uwezo wa kuingia katika utuuzima bila kuvurugwa utaratibu wa upatikanaji wa elimu.

Mradi huo unatekelezwa katika wilaya nne za Ngorongoro, Sengerema, Kasulu na Mkoani huko Pemba. Mkutano huo wa kamati ya ufundi ya mradi ulilenga kutoa ratiba ya utekelezaji wa mradi baada ya mada mbalimbali kuwasilishwa za utafiti uliofanyika na hali halisi iliyopo nchini kuhusu wasichana na wanawake kwa kuangalia sharia zilizopo, utamaduni na tabia. 
Akizungumza katika mkutano huo Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Huria (OUT) Kitivo cha Elimu, Dk. Felix Mulengeki alisema kwamba mradi huo utafanikiwa kutokana na ukweli kuwa sharia na katiba za nchi zipo vizuri huku sera nazo zikitambua haki ya kusoma. Ofisa wa Kitaifa anayeshughulikia Elimu ya Afya na Ukimwi ofisi za Unesco Dar es Salaam, Mathias Herman akiwasilisha taarifa ya mwaka 2017 ya mradi huo wakati wa mkutano wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.

Wakati mradi unabuniwa ilionekana kwamba kutoeleweka kwa katiba na sheria zilizopo zinazomlinda mtoto wa kike, uelewa hafifu umekuwa ukikwamisha maendeleo kielimu kwa watoto wa kike. Dk. Mulengeki alisema kwamba hali ya sera na sheria nchini Tanzania ni salama zaidi kilichobaki utekelezaji wa mradi huo umelenga kukusanya pia takwimu kwa ajili ya kutumika kutengeneza sera. 

  Katika mradi huo unatarajiwa kuongeza uelewa zaidi wa elimu ya afya ya uzazi na kutengeneza mifumo ya kuelimisha watu. Mada mbalimbali zilizojadiliwa ziliwezeshwa kupata muda wa utekelezaji wa vipengele mbalimbali ambavyo vilipaswa kufanyika ili kuondokana na tabia mbaya ambazo zinamnyima binti wa Kitanzania kukamilisha elimu yake. Washiriki wa kamati ya ufundi ya mradi wa KOICA unaowezesha wasichana na wanawake vijana kujiendeleza kielimu wakifuatilia ripoti ya mwaka 2017 ya mradi huo iliyokuwa ikiwasilisha Mathias Herman kwenye mkutano uliofanyika katika ofisi za Unesco jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO

yaani makala yote MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/mradi-wa-koica-kuwawezesha-mabinti.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MRADI WA KOICA KUWAWEZESHA MABINTI WAFANYA MKUTANO"

Post a Comment