MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA

MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA
kiungo : MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA

soma pia


MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifukuzia mbali kesi ya madai iliyofunguliwa na Dk.William Morris raia wa Marekani dhidi ya mke wake Dk.Phills Nyimbi na Mchungaji Josephat Mwingira kwa garama.

Dk.William Morris aliwasilisha maombi mahakamani hapo, akiomba, mkewe, Mwingira na mtoto wake (9) wafanyiwe kipimo cha DNA.Katika Maombi hayo Dk. Morris ambae ni mume wa (mdaiwa wa Pili, Philis Nyimbi) anaiomba Mahakama itoe amri ya mkewe Mwingira na mtoto wakafanyiwe kipimo hicho cha DNA.

Lengo ni kujua wazazi halisi wa mtoto aliyezaa na mkewe.Katika madai yake, Dkt. Morris anadai mchungaji Mwingira alizini na mkewe na hatimaye kuzaa naye mtoto wa kiume( 9).

Mapema mahakamani hapo,akisoma hukumu hiyo leo February 26 mwaka huu, Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba amesema Dk.Morris katika kesi hiyo ameshindwa kuonesha mahusiano ya kimapenzi kati ya Dk.Phills na Mchungaji Mwingira.

Pia ameshindwa kuthibitisha kuwa mtoto aliyezaliwa na mke wa Dk. Morris ni matokeo ya mahusiano ya kimapenzi kati ya Dk.Phills na Mchungaji Mwingira.Hivyo mahakama imeifukuzia mbali kesi hiyo ya madai na kueleza mdai ameshindwa kuthibitisha madai yake katika kiwango kinachotakiwa katika mashauri ya madai na alipe gharama.

"Si tu ameshindwa moja kwa moja lakini ameshindwa kiasi ambacho Mahakama hii inalazimika kutoa amri kuwa alipe garama walizotumia wadaiwa kwenye shauri hili" amesoma Hakimu Simba.Baada ya kutolewa kwa hukumu huyo Wakili wa mdai, Respicius Ishengoma amesema hawajaridhika na uamuzi huo na watakata rufaa.

Hukumu hiyo iliyoandaliwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mhini imesomwa leo nyakati za saa 8 mchana.Awali kwenye utetezi wa Dk.Phills Nyimbi aliieleza Mahakama hiyo hajawahi kuwa na uhusiano na Mchungaji Josephat Mwingira.



Hivyo makala MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA

yaani makala yote MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/mchungaji-mwingira-aibuka-kidedea.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MCHUNGAJI MWINGIRA AIBUKA KIDEDEA"

Post a Comment