MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI

MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI
kiungo : MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI

soma pia


MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI

Na Stella Kalinga-Simiyu

Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imeshauriwa kuwekeza katika kiwanda cha kutengeneza bidhaa za ngozi ikiwemo viatu, mikoba na mikanda kinachomilikiwa na kikundi cha Usindikaji Ngozi Senani kilicho kata ya Senani wilayani Maswa, ili kuongeza thamani ya ngozi zitokanazo na mifugo.

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda vidogo katika wilaya MASWA.

Mtaka amesema katika kutekeleza Sera ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Tanzania ya Viwanda , Halmashauri ya Maswa inapaswa kuwekeza katika viwanda vinavyoanzishwa na vikundi ili kuviwezesha katika upatikanaji wa malighafi ya kutosha, kuongeza thamani ya mazao ya mifugo pamoja na kilimo ili viwanda hivyo viweze kuzalisha kwa tija.

“Tungehitaji kuwa mkoa ambao utawekeza sana katika viwanda vidogo na ndiyo maana tulianza dhana ya Wilaya moja bidhaa moja kiwanda kimoja na sasa tunakwenda kwenye Kijiji Kimoja Bidhaa Moja Kiwanda kimoja; tunataka kupunguza uagizwaji wa bidhaa kutoka nje ya Mkoa” alisema Mtaka.Aidha, ameitaka Halmashauri hiyo kuwasaidia wanakikundi kuweka mifumo mizuri ya kutengeneza soko la bidhaa zinazozalishwa katika kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kuuza katika minada yote ya wilaya hiyo na kuimarisha soko la nje.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Dkt.Fredrick Sagamiko amesema Halmashauri itahakikisha kiwanda hicho kinapata malighafi ya kutosha ambapo amebainisha kuwa Halmashauri imeingia mkataba na Chuo cha DIT Mwanza kuhakikisha kuwa inazalisha malighafi(ngozi) kwa wakati kwa ajili ya kiwanda hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akivaa viatu vilivyotengenezwa katika Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za Ngozi kilichopo Senani Wilayani Maswa wakati wa Ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka(wa tatu kushoto) akiwa pamoja na viongozi wakuu wa Wilaya ya Maswa wakielekea katika Kiwanda kidogo cha kutengeneza bidhaa Ngozi katika Kijiji cha Senani kata ya Senani wakati wa ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akifuatilia hatua mbalimbali za utengenzaji wa viatu vya ngozi kwenye kiwanda cha kutengeneza bidhaa ngozi kilichopo Kijiji cha Senani kata ya Senani wakati wa ziara yake ya kukagua viwanda vidogo wilayani Maswa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kushoto) akizungumza na baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Njiapanda wilayani Maswa, wakati alipotembelea eneo ambalo kitajengwa kiwanda kidogo cha kutengeneza ungalishe kitakachomikiwa na shule za Msingi 30 za Maswa,wakati wa ziara yake ya kutembelea viwanda vidogo wilayani humo.




Hivyo makala MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI

yaani makala yote MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/maswa-yashauriwa-kuwekeza-kiwanda-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "MASWA YASHAURIWA KUWEKEZA KIWANDA CHA BIDHAA ZA NGOZI"

Post a Comment