title : MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA
kiungo : MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA
MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na Ujumbe wa Mawaziri wawili kutoka Malawi na kuzungumza kuhusu uwezekano wa Malawi kupata Gesi Asilia kutoka Tanzania na Uendelezaji wa pamoja wa Bonde la Mto Songwe kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo uzalishaji umeme.
Ujumbe wa Malawi uliongozwa na Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa ambao waliambatana na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe na wataalam kutoka Taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara zao.
Waziri Kalemani alikutana na ujumbe huo Februari 12, 2018 katika Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam ambapo alielezwa dhumuni la ziara hiyo ya Mawaziri hao wawili kutoka nchini Malawi.
Akizungumza katika mkutano huo, Waziri wa Nishati wa Malawi, Aggrey Masi alisema kuwa Malawi inaupungufu mkubwa wa nishati ya umeme na kwamba jitihada mbalimbali zinafanyika kuhakikisha kiwango cha uzalishaji umeme kinaongezeka.
Mawaziri kutoka Malawi mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa ajili ya majadiliano kuhusu masuala ya Nishati na mwenyeji wao Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Kushoto ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi na Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa.
Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya Nishati na Mawaziri kutoka Malawi (hawapo pichani).
Ujumbe wa Mawaziri kutoka Malawi ukiendelea na majadiliano wakati wa mkutano na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini, Aggrey Masi, Waziri wa Viwanda, Biashara na Utalii, Henry Mussa na Balozi wa Malawi nchini, Hawa Ndilowe.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akizungumza jambo wakati wa mkutano na Mawaziri kutoka Malawi. Kulia ni Waziri wa Maliasili, Nishati na Madini wa Malawi, Aggrey Masi.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA
yaani makala yote MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/malawi-yaonesha-nia-kupata-gesi-kutoka.html
0 Response to "MALAWI YAONESHA NIA KUPATA GESI KUTOKA TANZANIA"
Post a Comment