title : Makamu Mwenyekiti wa UWT afanya ziara katika Mkoa wa Magharibi Unguja
kiungo : Makamu Mwenyekiti wa UWT afanya ziara katika Mkoa wa Magharibi Unguja
Makamu Mwenyekiti wa UWT afanya ziara katika Mkoa wa Magharibi Unguja
Na Is-Haka Omar, Zanzibar.
VIONGOZI na watendaji wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT) Tanzania wameshauriwa kuendeleza utamaduni wa kuwatembelea wananchi ili kuibua kero zinazowakabili na kuzifanyia kazi kwa mujibu wa matakwa ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.
Pia wametakiwa kuzitendea haki dhamana za uongozi walizonazo katika medali za kisiasa kwa kuhakikisha CCM inazidi kuwa Chama bora na imara chenye sera , taratibu na misingi ya maadili yanayokidhi matakwa ya wananchi wote bila ya ubaguzi wa kidini na kikabila.
Ushauri huo umetolewa kwa wakati tofauti na Waasisi na viongozi wa zamani wa UWT katika mwendelezo wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo Taifa Ndugu Thuwayba Kisasi, katika Mkoa wa Magharibi Unguja.
Akizungumza mwasisi wa UWT aliyewahi kushika nyadhifa mbali mbali ndani Umoja huo na Mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa CCM Taifa Bi.Mariam Hengwa (75) hapo nyumbani kwake kwa Mchina mwisho, amesema Chama Cha Mapinduzi kipo ngazi za chini kwa wananchi hivyo viongozi hao wapange utaratibu wa kuwatembelea wananchi mara kwa mara.
Bi. Mariam amesema viongozi wa UWT wanatakiwa kubuni mipango mbali mbali ya kimaendeleo itakayoongeza Ari na utendaji kwa Akina Mama wa Umoja huo, na kuwavutia wanawake wa upinzani kujiunga na CCM.
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa, Thuwayba Kisasi (kushoto) akisikiliza kwa makini nasaha za muasisi wa UWT Bi. Salama Majaliwa alipotembelewa nyumbani kwake Mwera na uongozi wa Umoja huo.
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa, Thuwayba Kisasi (kushoto) akisikiliza kwa makini nasaha za muasisi wa UWT, Bi. Mariam Hengwa(aliyekuwa katikati akizungumza) alipotembelewa na UWT yumbani kwake Kwa mchina-Mombasa Unguja.
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa, Thuwayba Kisasi (kulia) akisikiliza kwa makini nasaha za muasisi wa UWT, Bi. Rufea Juma Mbarouk(kushoto) alipotembelewa na UWT nyumbani kwake Mbweni Unguja.
MAKAMU Mwenyekiti wa UWT Taifa, Thuwayba Kisasi (kulia) akimkabidhi zawadi muasisi wa UWT, Bi. Rufea Juma Mbarouk(kushoto) alipotembelewa na UWT nyumbani kwake Mbweni Unguja.
Hivyo makala Makamu Mwenyekiti wa UWT afanya ziara katika Mkoa wa Magharibi Unguja
yaani makala yote Makamu Mwenyekiti wa UWT afanya ziara katika Mkoa wa Magharibi Unguja Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Makamu Mwenyekiti wa UWT afanya ziara katika Mkoa wa Magharibi Unguja mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/makamu-mwenyekiti-wa-uwt-afanya-ziara.html
0 Response to "Makamu Mwenyekiti wa UWT afanya ziara katika Mkoa wa Magharibi Unguja"
Post a Comment