MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO

MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO
kiungo : MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO

soma pia


MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO

Na Veronica Simba – Loliondo
Serikali imewaahidi wakazi wa Kata ya Mundarara katika Wilaya ya Longido kuwa itahakikisha madini ya Ruby ambayo yanapatikana katika eneo hilo yanaendelea kuwanufaisha na siyo kuwadidimiza.
Ahadi hiyo ilitolewa jana, Februari 13 na Naibu Mawaziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Dotto Biteko baada ya kufanya ziara katika Mgodi unaojishughulisha na uchimbaji wa madini hayo na kisha kuzungumza na wananchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, Nyongo na Biteko waliwataka wananchi wa Mundarara kuondoa hofu kuwa neema ya madini hayo yanayopatikana katika maeneo yao haitawanufaisha tena kutokana na kile wanachodai kuwa sheria mbalimbali zilizowekwa na Serikali zinasababisha kupungua kwa Soko lake.
Akizungumza na wananchi hao, Naibu Waziri Biteko aliwaambia kuwa, Serikali kupitia Wizara ya Madini inaandaa mwongozo maalum utakaobainisha utaratibu unaopaswa kutumika katika biashara ya kila aina ya madini hapa nchini ili yaweze kuwanufaisha wananchi na Taifa ipasavyo.
“Nia ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha rasilimali zote zinazopatikana nchini yakiwemo madini, zinalinufaisha Taifa kwa kiwango kinachostahili. Kwa muda mrefu tumekuwa tukiibiwa sana na watu wengine kunufaishwa na rasilimali zetu wenyewe ilhali sisi tunazidi kuwa maskini. Sasa tumeamua kuwa hatutaki kuibiwa tena,” alisisitiza.
Akifafanua zaidi, Biteko alisema kwamba, mwongozo huo unaoandaliwa na Serikali utasaidia hata wananchi wanaozungukwa na Migodi ya Madini kunufaika zaidi.
Naibu Waziri wa Madini Dotto Biteko akizungumza na wananchi wa Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido, baada ya kufanya ziara katika Mgodi unaochimba madini ya Ruby eneo hilo Februari 13 mwaka huu. Biteko aliambatana na Naibu Waziri Stanslaus Nyongo (hayupo pichani)
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo akizungumza na wananchi wa Kata ya Mundarara Wilaya ya Longido, baada ya kufanya ziara katika Mgodi unaochimba madini ya Ruby katika eneo hilo, Februari 13 mwaka huu. Nyongo aliambatana na Naibu Waziri Dotto Biteko (hayupo pichani)
Sehemu ya umati wa wananchi wa Kata ya Mundarara wilayani Longido, wakiwa katika Mkutano wa Naibu Mawaziri wa Madini Stanslaus Nyongo na Dotto Biteko (hawapo pichani), walipofanya ziara katika Mgodi unaochimba madini ya Ruby katika eneo hilo, Februari 13 mwaka huu na kuzungumza nao.
Naibu Mawaziri wa Madini Dotto Biteko na Stanslaus Nyongo wakizungumza na wawekezaji wa Mgodi wa Madini ya Ruby katika Kijiji cha Mundarara wilayani Longido, Februari 13 mwaka huu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO

yaani makala yote MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/madini-ya-ruby-kuendelea-kuwanufaisha.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MADINI YA RUBY KUENDELEA KUWANUFAISHA WANANCHI LONGIDO"

Post a Comment