JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma.

JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma.
kiungo : JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma.

soma pia


JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma.

Wazazi wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanapata chanjo

zote zinazotakiwa ili waweze kuepukana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo.




Rai hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia

wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiongea na wabunge

waliohudhuria semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza

iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo

ilifanyika katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.




Waziri Ummy aliwaomba wabunge hao kila wanapokutana na wananchi

kupitia mikutano ya hadhara wawasisitize umuhimu wa kuwapeleka watoto

wao katika vituo cha afya ili wakapate chanjo zinazohitajika kwa

wakati.




Aidha Waziri huyo alisema kuwa matibabu ya moyo pamoja na magonjwa

mengine yasiyoambukiza ni ya gharama kubwa na kuwaomba wabunge hao

kuwahimiza wananchi kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambao

utawasaidia kupata matibabu katika Hospitali zote nchini ikiwemo JKCI

na Hospitali ya Taifa Muhimbili.




Katika hatua nyingine Mhe. Ummy aliwataka wakurugenzi wa Taasisi

zingine kuiga mfano wa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya

Kikwete Prof. Mohamed ambaye kupitia uongozi wake na jitihada zake

binafsi Taasisi hiyo imeweza kutoa huduma bora na kuwahudumia wananchi

vizuri katika matibabu ya moyo na hivyo kuokoa maisha ya watanzania

wengi.


 Mbunge wa Lupa Mhe. Victor Mwambalaswa akiwasisitiza wabunge
wenzake umuhimu wa kupima afya zao hasa tezi dume kwa wanaume wakati wa semina
ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo
Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.



 Mbunge wa  Bunda mjini  Mhe. Ester Bulaya akieleza jinsi
anavyoridhishwa  na huduma za matibabu ya
moyo zinazotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati wa semina ya
afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza iliyoandaliwa na JKCI ambayo ilifanyika
jana  katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini
Dodoma.



 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia wazee na Watoto
Mhe. Ummy Mwalimu akielezea mpango wa Serikali kupitia Hospitali za mikoa wa
kusomesha madaktari bingwa wengi ili kuweza kukabiliana na uhaba wa wataalam  hao wakati wa  semina ya afya ya moyo na magonjwa
yasiyoambukiza iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo
ilifanyika jana   katika ukumbi wa Pius
Msekwa mjini Dodoma. Kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Huduma za Maendeleo ya
Jamii Mhe. Peter Serukamba.



 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)
Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Daktari wa Bunge Jeminian Temba mara baada
ya kumalizika kwa semina ya afya ya moyo na magonjwa yasiyoambukiza
iliyoandaliwa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambayo ilifanyika jana   katika ukumbi wa Pius Msekwa mjini Dodoma.
Katikati ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo Yona Gandye.





Hivyo makala JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma.

yaani makala yote JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/jkci-yafanya-semina-ya-afya-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JKCI yafanya semina ya afya ya moyo,magonjwa yasiyoambukiza kwa Wabunge mjini Dodoma."

Post a Comment