title : JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO
kiungo : JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO
JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO
Na Luteni Selemani Semunyu JWTZ
MKUU wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo amewataka wachezaji wa Gofu wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo kuhakikisha wanarejesha heshma ya jeshi kwa kuwa kinara katika michezo na kuzalisha wachezaji bora wanaowakilisha nchi kimataifa.
Aliyasema hayo Makao Makuu ya Jeshi Upanga jijini Dar es Salaam wakati akiagana na wachezaji Sita wa Gofu wanaotarajia kuwakilisha nchi katika michuano ya wazi ya wanawake nchini Nigeria IBB Ladies Open Championship 2018 yanayaotarajia kufanyika hivi karibuni.
Jenerali Mabeyo amesema kama ilivyokuwa katika michezo ya iiadha na ngumi sasa tunataka na kwenye gofu na kwa kuanza ni timu hii ya Gofu ya Wanawake kuhakikisha inarudi na ushindi mnono.
“ Nikiwa mlezi wa Klabu naamini mtatuwakilisha vyema na Jeshi kwa ujumla tutaendelea kuwaunga mkono wachezaji wa Gofu na hata Michezo mingine kuhakikisha jeshi linaendelea kuwa kinara w michezo nchini na kuwa chachu kwa wengine,” alisema Jenerali Mabeyo.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akimkabidhi Bendera ya taifa Nahodha wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo inayotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria Hivi karibuni.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo akiwa katika Picha ya Pamoja na Wachezaji na Viongozi wa Klabu ya Gofu ya jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania ya Lugalo Wakuu wa Matawi na Wachezaji wanaotarajia kushiriki mashindano ya Wazi ya Wanawake ya IBB nchini Nigeria hivi karibuni.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO
yaani makala yote JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/jenerali-mabeyo-awataka-wachezaji-wa.html
0 Response to "JENERALI MABEYO AWATAKA WACHEZAJI WA GOFU LUGALO KUREJESHA HESHIMA KWA KUWA VINARA WA MCHEZO HUO"
Post a Comment