title : HUKUMU KESI YA MASOGANGE KUTOLEWA FEBRUARI 21 MWAKA HUU
kiungo : HUKUMU KESI YA MASOGANGE KUTOLEWA FEBRUARI 21 MWAKA HUU
HUKUMU KESI YA MASOGANGE KUTOLEWA FEBRUARI 21 MWAKA HUU
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu Februari 21 mwaka huu, inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya matumizi ya dawa za kulevya inayomkabili Video Qeen Agnes Gerald 'Masogange'
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ndio atakayesoma hukumu hiyo baada ya upande wa mashtaka uliowakilishwa na Wakili wa Serikali, Costantine Kakula kuwaita mashahidi watatu kutoa ushahidi dhidi ya Masogange na kuufunga huki mshtakiwa akijitetea mwenyewe.
Kabla ya kutolewa kwa tarehe ya hukumu, Masogange akiongozwa na Mawakili wake, Nehemiah Nkoko na Ruben Simwanza, ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuachie huru kwa sababu hana kosa lolote.
Akitotoa utetezi wake,Leo mahakamani hapo Masogange anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam, amedai yeye hajawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja.
Amedaimbali ya kuwa Video Qeen yeye alikuwa ni mfanyabiashara wa nguo.
Alidai Februari 14, mwaka jana polisi walipoenda nyumbani kwake, yeye hakuwepo, alikuwepo dada yake, yeye alikuwa amempeleka mjomba wake kununua vitu Ocadeco.
Alidai, Polisi hao walimuweka chini ya ulinzi dada yake na kumtaka ampigie simu na ajifanye anaumwa ili arudi nyumbani lakini baada ya kupigiwa simu, alirudi nyumbani Kwake saa 12 jioni.
Ambapo alipofika getini kabla hajashuka kwenye gari alimuona mlinzi amekaa na watu wanne, aliwasalimia na kuingia ndani.
Aliendelea kudai ilipofika ndani alimkuta dada yake na askari wa kike na askari wawili wa kiume, walimueleza wanasubiri yeye na wakajitambulisha kuwa wao ni polisi ambao walimuuliza kuwa wamekwenda kufanya upekuzi,
Alidai baada ya upekuzi huo, alichukuliwa na kupelekwa kituo cha polisi cha kati na walipofika mapokezi akaandikisha jina na wakampeleka rumande ambapo alikaa siku tisa.
Alidai baada ya mahojiano polisi alipelekwa Mwananyamala ambapo alioneshwa picha mbili za wanaume wawili, akaulizwa kama anawafahamu na kuwaeleza kuwa hawafahamu.
Alidai baada ya hapo alipelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na kupimwa mkojo akiwa chini ya ulinzi wa askari wa kike, afande Judy na baadae akarudishwa Polisi.
" Mheshimiwa Mimi sijawahi kutumia dawa za kulevya hata siku moja nipo tayari hata mahakama yako ijiridhishe kwa kunipima." alieleza Masogange.
Katika kesi hiyo Masogange anadaiwa kati ya February 7 na 14,mwaka 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).
Pia anadaiwa kati ya February 7 na 14, mwaka 2017 alitumia dawa za kulevya aina ya Oxazepam
Hivyo makala HUKUMU KESI YA MASOGANGE KUTOLEWA FEBRUARI 21 MWAKA HUU
yaani makala yote HUKUMU KESI YA MASOGANGE KUTOLEWA FEBRUARI 21 MWAKA HUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HUKUMU KESI YA MASOGANGE KUTOLEWA FEBRUARI 21 MWAKA HUU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/hukumu-kesi-ya-masogange-kutolewa.html
0 Response to "HUKUMU KESI YA MASOGANGE KUTOLEWA FEBRUARI 21 MWAKA HUU"
Post a Comment