title : DC KIBAHA ATOA SIKU 90 MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI KIJIJI CHA LUKENGE
kiungo : DC KIBAHA ATOA SIKU 90 MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI KIJIJI CHA LUKENGE
DC KIBAHA ATOA SIKU 90 MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI KIJIJI CHA LUKENGE
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI
SERIKALI wilayani Kibaha,Mkoa wa Pwani imemtaka mwekezaji ambaye alichukua eneo lenye ukubwa wa hekari zipatazo 5000 za ardhi bila ya kuzingatia sheria na taratibu kuzirudisha kwa kipindi cha siku tisini kutokana na kushindwa kuliendeleza kwa kipindi cha zaidi ya miaka nane kama walivyokubaliana katiba mkataba na wananchi wa kijiji cha lukenge kata ya Magindu.
Sakata la mgogoro wa ardhi baina ya wananchi hao na mwekeaji limechukua sura mpya kufuatai Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi hivyo kumtaka mwekezaji huyo kuzirudisha hekari hizo 5000 kwa wananchi ambazo alikuwa amepewa na serikali ya kijiji kwa ajili ya uwekezaji wa ufugaji wa kisasa wa ng’ombe pamoja na samaki lakini ameshindwa kutekeleza makubaliano aliyopatiwa hapo awali.
Akizungumza katika mkutano maalumu wa adhara ambao uliandaliwa kwa ajili ya kujadili sakata hilo Mkuu huyo wa Wilaya amesema eneo hilo mwekezaji huyo alipewa kwa ajili ya kuliendeleza lakini amekuwa akijinufaisha mwenywe na kuwanyonya wakazi wa eneo hilo bila ya kuwaletea maendeleo ya aina yoyote tofauti na makubaliano yao.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akizungumza na umati wa wananchi wa kijiji cha Lukenge kata Magindu hawapo pichani katika mkutano wa adhara ambao aliuandaa kwa ajili ya kuweza kutatua mgogoro wa aradhi kati ya wananachi hao na mwekezaji ambao umedumu kwa kipindi kirefu
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama akiwa anatoka kwenye mkutano na wananchi wa kijiji cha lukenge alipokwenda kwa ajili ya kumaliza sakata la mgogoro baina ya wananachi hao pamoja na mwekezaji.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha lukenge wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama wakati wa mkutano wa adhara ambao uliandaliwa kwa ajili ya kusikiliza mgogoro uliopo katia ya wananchi na mwekezaji.
Wananchi wa kijiji cha lukenge wakiwa wameshika mabango yaliyokuwa yameandikwa ujumbe wa kumkataa mwekezaji huyo, ambapo walipita mbele kwa ajili ya kuweza kumuonyesha Mkuu wa Wilaaya ya Kibaha.
PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU
Hivyo makala DC KIBAHA ATOA SIKU 90 MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI KIJIJI CHA LUKENGE
yaani makala yote DC KIBAHA ATOA SIKU 90 MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI KIJIJI CHA LUKENGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DC KIBAHA ATOA SIKU 90 MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI KIJIJI CHA LUKENGE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/dc-kibaha-atoa-siku-90-mwekezaji.html
0 Response to "DC KIBAHA ATOA SIKU 90 MWEKEZAJI KURUDISHA HEKARI 5000 KWA WANANCHI KIJIJI CHA LUKENGE"
Post a Comment