Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni

Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni
kiungo : Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni

soma pia


Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni

 Balozi wa Tanzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika yeye na Mwenzake Balozi Muhidin Ali Mboweto anayekwenda Nigeria walipofika kuaga rasmi. Kati kati yao ni Balozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Nigeria  Muhidin Ali Mboweto.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Balozi Muhidin Ali Mboweto Kushoto na Balozi wa Tanzania Nchini Sweden Dr. Wilbrod Slaa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Dr. SlaaKulia na Balozi Seif Kulia wakifanyiana mzaha walipokuwa wakikumbushana utumishi wao wakati walipokuwa Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya M,uungano wa Tanzania mara baada ya mazungumzo yao.

Na Othman Khamis , OMPR


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alikutana kwa mazungumzo na Mabalozi  Muhidin Ali Mboweto  anayeiwakilisha Tanzania Nchini Nigeria na Dr. Wilbrod Slaa anayekwenda Nchini Sweeden walipofika Ofisini kwake kumuaga rasmi wakielekea katika vituo vyao vya kazi walivyopangiwa.
Katika mazungumzo yao Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaeleza Mabalozi hao kwamba nafasi ya Ubalozi ni fursa nzito ya Uwakilishi wa Nchi inayopaswa kutumikiwa kwa uzalendo wa hali ya juu.
Balozi Seif  aliwaeleza Mabalozi hao wa Tanzania kwamba Nigeria na Sweeden ni Nchi zenye Historia kubwa ya ushirikiano na Tanzania inayopaswa wasimamizi hao wa Diplomasia kuangalia maeneo ambayo yanaweza kuendelea kudumisha Uhusiano huo.
Alisema zipo sekta ambazo Nigeria na Sweeden zinaweza kuisaidia Zanzibar Kitaaluma akitolea Mfano eneo la Utalii, Umeme Mbadala na hata masuala ya Uhifadhi wa Nyaraka kwa vile Mataifa hayo tayari yameshapiga hatua kubwa Kitaaluma.
Mapema Balozi wa Tananzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa kwa niaba ya mwenzake Balozi Muhidin Ali Mboweto anayekwenda Nigeria alisema wanajitambua kwamba wao  ni Wawakilishi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Dr. Slaa alimueleza Balozi Seif kwamba utumishi wao wa Kidiplomasia watauelekeza zaidi katika Diplomasia ya Kiuchumi kama Dunia ilivyobadilika kujikiota zaidi katika eneo hilo.



Hivyo makala Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni

yaani makala yote Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/balozi-seif-akutana-na-mabalozi-wapya.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Balozi Seif akutana na Mabalozi wapya walioteuliwa karibuni"

Post a Comment