title : BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR,MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO
kiungo : BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR,MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO
BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR,MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kulipa ushirikiano wa kina Jeshi la Polisi Nchini katika kuona Amani ya Taifa pamona na Raia wake inaendelea kudumu muda wote.
Alisema Zanzibar ina changamoto nyingi zikiwemo za Kisiasa, Dawa za Kulevya na ukosefu wa Maadili unaopelekea kuibuka kwa kasi zaidi ya Udhalilishaji wa Kijinsia ambazo zinahitaji kushughulikiwa ipasavyo ili kuleta ustawi na Utulivu.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakati akizungumza na Kamishna Mpya wa Polisi Zanzibar Mohamed Haji Hassan aliyefika kujitambulisha Rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli hivi karibuni.
Balozi Seif alisema masuala ya udhalilishaji pamoja na Dawa za kulevya hivi sasa yamekithiri na kuleta sura mbaya ndani ya Jamii kiasi cha kulazimika kutungwa sheria ili kujaribu kupambana na kadhia hiyo inayotoa picha mbaya katika uso wa Dunia.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliviagiza vyombo vya Dola kuwasaka na baadae kuwashughulikia ipasavyo wale wote wanaohusika na uingizaji wa Dawa za Kulevya Nchini kwa vile wao ndio chanzo cha balaa zote zinazotokea katika Mitaa mbali mbali Nchini.
Hata hivyo Balozi Seif alikemea tabia ya baadhi ya Maofisa wa Vyombo vya Dola kujaribu kufifilisha kesi za Dawa za kulevya kwa kuwapa afuweni Watuhumiwa huku wakizingatia zaidi kupokea Rushwa badala ya kuwaonea huruma wale wanaoathirika kutokana na wimbi la Dawa hizo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kulia akizungumza na Kamishna Mpya wa Polisi Zanzibar Mohamed Haji Hassan alipofika Ofisini kwake Vuga kujitambulisha rasmi baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Balozi wa Tanzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa Kushoto akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika yeye na Mwenzake Balozi Muhidin Ali Mboweto anayekwenda Nigeria walipofika kuaga rasmi. Kati kati yao ni Balozi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini Nigeria Muhidin Ali Mboweto.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kati kati akizungumza na Balozi wa Tanzania Nchini Nigeria Balozi Muhidin Ali Mboweto Kushoto na Balozi wa Tanzania Nchini Sweeden Dr. Wilbrod Slaa Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Dr. Slaa Kulia na Balozi Seif Kulia wakifanyiana mzaha walipokuwa wakikumbushana utumishi wao wakati walipokuwa Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya M,uungano wa Tanzania mara baada ya mazungumzo yao.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR,MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO
yaani makala yote BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR,MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR,MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/02/balozi-seif-akutana-na-kamishna-mpya-wa.html
0 Response to "BALOZI SEIF AKUTANA NA KAMISHNA MPYA WA POLISI ZANZIBAR,MABALOZI DR. SLAA NA MBOWETO"
Post a Comment